MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
Kusoma na Kuandika kwa madhumuni mbalimbali - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
Kusoma na Kuandika kwa madhumuni mbalimbali - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3)
+---- Forum: Stashahada/Cheti (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=21)
+----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=25)
+----- Thread: Kusoma na Kuandika kwa madhumuni mbalimbali (/showthread.php?tid=702)



Kusoma na Kuandika kwa madhumuni mbalimbali - MwlMaeda - 08-01-2021

Kusoma na Kuandika kwa madhumuni mbalimbali
Sehemu ya 1: Kuhamasisha na kutathmini usomaji na uandishi
Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuhamasisha ujifunzaji kusoma na kuandika na kutathmini maendeleo?
Maneno muhimu: kujua kusoma na kuandika katika hatua za mwanzo; nyimbo; mashairi; chapa za kimazingira; tathmini; kazi ya kikundi; usomaji wa ushirika.
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
  • kutumia nyimbo na mashairi kufundisha wanafunzi wa kiwango cha mwanzo kusoma;
  • kutumia ‘chapa za kimazingira’ na bidhaa za dukani kufundishia usomaji, uandishi na uchoraji;
  • kutalii njia za kuhamasisha ujifunzaji kwa kutumia kazi ya kikundi;
  • kukuza uwezo wako wa kutathmini ujifunzaji.
Utangulizi
Msomaji na mwandishi mfanisi anatakiwa ajue na aweze kufanya nini? Kama mwalimu, unatakiwa uweze kujibu swali hili ili uweze kuwaongoza wanafunzi wako. Kujifunza kusoma na kuandika kwa ufanisi kunahitaji mazoezi. Hivyo, ni muhimu kutumia mikabala na shughuli mbalimbali ambazo zitawafanya wanafunzi wafurahie. Ni muhimu kutathmini maendeleo ya wanafunzi na kujiuliza mwenyewe kama unakidhi matakwa yao. Sehemu hii inatalii mawazo haya kwani inaangalia ujifunzaji kusoma na kuandika katika hatua za awali.
Somo la 1
Kujifunza kusoma na kuandika ni kazi ngumu! Kwa sababu unataka wanafunzi wazingatie masomo ya kusoma na kuandika, ni muhimu ufanye darasa lako –na shughuli ambazo zinahamasisha ujifunzaji kusoma na kuandika –liwe la kusisimua kadiri iwezekanavyo.
Nyenzo Rejea 1: Wanachotakiwa kukijua wale wasomaji na waandishi wafanisi inaeleza kwamba wanafunzi wanahitaji kujua jinsi ya kuhusisha sauti na herufi, herufi na maneno, maneno na sentensi. Nyimbo na mashairi ambayo wanafunzi wanayajua vizuri –na ambayo wanaweza kuyaimba na kuyaghani kwa kuonesha vitendo –yanawasaidia kujenga mahusiano haya. Pia kushirikishana na wanafunzi wako katika usomaji wa kitabu cha hadithi chenye chapa kubwa kunajenga mahusiano. Unapokuwa unasoma, acha kuwaonesha kila picha na waulize wanafikiri kitu gani kitatokea au kitafuata baadaye. Unapokuwa umemaliza, tumia hiki kitabu kwa shughuli za ugunduzi wa herufi na maneno ambazo utawaambiwa wanafunzi wenyewe waonesha na wasome herufi na maneno fulani. Kumbuka kuwapatia wanafunzi fursa nyingi ili wazungumzie kuhusu hadithi hii –wahusika, kilichotokea, wanavyojisikia kuhusiana na hadithi n.k.
Uchunguzi kifani ya 1: Kuwapatia wanafunzi utangulizi kuhusu usomaji
Bibi Nomsa Dlamini anafundisha wanafunzi wa darasa la 1 wa Nkandla, Afrika Kusini, kusoma na kuandika KiisiZulu. Nomsa huwasomea vitabu vya hadithi, kutoka kwenye baadhi ya vitabu alivyoandika na kufafanua mwenyewe kwa sababu vipo vitabu vichache vya KiisiZulu.
Mwanzoni mwa mwaka, anahakikisha kwamba kila mwanafunzi anaelewa jinsi kitabu kilivyotungwa –jalada, jina la kitabu, hadithi ilivyojengwa –kwa sababu anajua kuwa baadhi yao hawakuwahi kushika kitabu kabla ya kuanza shule. Amegundua kwamba utabiri wa shughuli, ambapo wanafunziwanapendekeza kile kitakachofuata katika hadithi, una umuhimu na huchangamsha wanafunzi wake.
Nomsa amegundua kwamba wanafunzi wanahitaji mazoezi mengi ili kuwafanya wajiamini katika usomaji. Hutengeneza nakala nyingi za machapisho ya mashairi au nyimbo za KiZulu ambazo wanazijua vizuri na nyingine ambazo anajua kuwa ni mahsusi kwa ajili ya ufundishaji wa ugunduzi wa herufi-sauti. Wanafunzi huzisema au huziimba na kuonesha vitendo kuhusiana na nyimbo na mashairi hayo (angalia Nyenzo Rejea 1: Mifano ya nyimbo na mashairi ). La muhimu zaidi, aliwaambia wanafunzi wenyewe waguse na kusoma herufi na maneno. Baadhi ya wanafunzi waliona kuwa kazi hii ni ngumu hivyo alinukuu majina yao na herufi au maneno waliyoona yanawapa shida. Aliandaa kadi zenye picha, herufi na maneno ili kuzitumia kwa njia nyingine na wanafunzi hawa, ama kwa mmojammoja au katika vikundi vidogovidogo, wakati wanafunzi wengine wakiwa wanafanya shughuli nyingine. Nomsa anafarijika kuona kuwa zoezi hili lilisaidia katika kuwafanya wanafunzi hawa wajiamini na kusonga mbele.
Shughuli ya 1: Kutumia nyimbo na mashairi katika kufundisha usomaji
Waambie wanafunzi:
Wachague wimbo au shairi wanalolipenda;
wauimbe/waghani;waangalie kwa makini, unaposema maneno na kuyaandika ubaoni (au kwenye karatasi /ubao ili uweze kuyatumia tena);wasome wimbo/shairi ulilonalo (fanya hivi mara nyingi);waoneshe kwa kugusa herufi fulani (mojamoja) au maneno au alama za uandishi (herufi kubwa, kituo, alama ya kuuliza);waamue vitendo mtakavyofanya mkiwa mnaimba wimbo/kughani shairi ; wafanye vitendo hivi mkiwa mnaimba tena wimbo/kughani tena shairi; wakae kwenye vikundi vya wannewanne na mpeane zamu za kusomeana wimbo huu/shairi hili.
Zunguka darasani, ukiangalia wanafunzi wanaopata matatizo katika usomaji.
Malizia kwa kuliambia darasa zima liimbe tena wimbo au lighani tena shairi, na kuonesha vitendo.
Somo la 2
Baadhi ya wanafunzi wanakulia katika nyumba ambazo zina utajiri wa chapa na maumbo: maboksi ya bidhaa za dukani, pakiti na makopo, vitabu kwa ajili ya watoto na watu wazima, magazeti hata kompyuta/ngamizi. Wengine wana vifaa hivi kwa uchache nyumbani kwao. Changamoto yako kama mwalimu ni kulipatia darasa lako mazingira yenye utajiri wa chapa . Njia moja ya kufanya hivi ni kukusanya vifaa vyovyote popote vinapopatikana. Vifaa vya kufungashia (maboksi ya mbao, pakiti na makopo) mara nyingi vinaandikwa sana na hata wanafunzi wadogo mara nyingi hutambua maneno muhimu kwa zile bidhaa ambazo zinatumika sana nyumbani. Kwa wasomaji wazoevu, magazeti ambayo wanajumuiya wameshamaliza kuyasoma yanaweza kutumiwa kwa shughuli nyingi darasani.
Sehemu hii inatalii njia za kutumia chapa kama hizi katika kusaidia kujifunza kusoma.
Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia orodha ya vitu vya dukani kwa shughuli za kujifunza kusoma na kuandika
Precious Muhaji hufundisha Kiingereza kwa wanafunzi 45 wa Darasa la 4 lililopo Lushoto katika Milima ya Usambara. Hawajazoea sana Kiingereza lakini wanatambua herufi na baadhi ya maneno ya Kiswahili yaliyopo kwenye vifaa vya kuhifadhia bidhaa ndogondogo za nyumbani.
Precious alimwomba jirani yake maboksi/makasha, pakiti na makopo matupu. Alivileta vitu hivi shuleni ili kuvitumia katika shughuli za kujifunza kusoma na kuandika.
Mchezo unaopendwa na wanafunzi wake ni mchezo wa ‘ugunduzi wa maneno’. Precious alilipanga darasa katika vikundi tisa vya wanafunzi watanowatano na kukipa kila kikundi boksi, pakiti au kopo lilelile. Aliwaambia wanafunzi waandike namba kuanzia 1 mpaka 5 na kisha aliuliza maswali matano (angalia Nyenzo Rejea 3: Maswali ya mfano ya kuuliza kuhusu vitu vya nyumbani ). Wanafunzi walilinganisha majibu wenyewe na waliamua kuhusu jibu la kikundi. Precious alijadili yale maswali na darasa zima. ‘Mshindi’ alikuwa ni kikundi kilichomaliza cha kwanza na kuweza kutoa majibu sahihi zaidi.
Wakati mwingine Precious alikikaribisha kila kikundi ili kiweze kuuliza swali linalohusiana na ugunduzi wa neno.
Ili kuwahamasisha wanafunzi wafikiri kwa makini, wakati mwingine aliuliza swali kuhusu mchoro wa kifaa kinachohifadhia bidhaa na ujumbe uliopo kwenye tangazo.
Precious aligundua kuwa wanafunzi wengine hawakushiriki, hivyo wakati mwingine walipocheza mchezo huu, alimwambia kila mwanafunzi aandike maneno manne kutoka kwenye kontena la kuhifadhia bidhaa za dukani kabla ya kurudi kwenye viti vyao vya kawaida. Wakiwa wamesharudi kwenye viti vyao alimwambia kila mmoja amsomee mwenzake orodha yake. Aligundua wanafunzi sita ambao walihitaji msaada zaidi na alifanya nao kazi baada ya saa za shule kwa nusu saa, kwa kutumia vitu vilevile na kuwapatia muda wa kufanya mazoezi ya kubainisha herufi na maneno.
Precious aligundua kuwa kuzoea herufi na maneno katika vifaa vya kuhifadhia bidhaa huwasaidia wanafunzi kubainisha herufi na maneno haya katika matini nyingine walizozisoma, kama vile hadithi. Kwa kunakili maneno kutoka katika vitu hivyo, wanafunzi pia hujifunza kuandika herufi na maneno kwa kujiamini zaidi na kwa usahihi zaidi.
Shughuli ya 2: Kutumia orodha ya bidhaa za dukani kwa shughuli za usomaji na uandishi
Leta makopo/mikebe, pakiti au maboksi ya kutosha darasani ili kila kikundi cha wanafunzi watanowatano au sitasita kipate kitu kimojawapo cha kukifanyia kazi au liambie darasa lako likusaidie katika ukusanyaji wa vitu hivi.
Andika maswali ubaoni kuhusu maneno na picha zinazoonekana kwenye pakiti, kopo au boksi ( angalia Nyenzo Rejea 3 ). Ama waambie wanafunzi wayasome au uwasomee.
Ama chezesha mchezo wa ugunguzi wa maneno katika vikundi (angalia Uchunguzi Kifani 2) au waambie wanafunzi waandike majibu wenyewe. Panga muda wa ziada wa mazoezi na wa kutoa msaada zaidi kwa ajili ya wanafunzi ambao hawawezi shughuli hii.
Katika somo linalofuata, waambie wanafunzi wafanye kazi katika vikundi vilevile wabuni maandishi na taarifa zinazoonekana kwa ajili ya kifaa cha kweli au picha ya bidhaa za dukani.
Kiambie kila kikundi kioneshe na kuzungumzia kuhusu ubunifu/mchoro wao kwa wanafunzi wote darasani.
Wanafunzi wamejifunza nini kwa kusoma orodha ya bidhaa za dukani na kwa kuchora na kuonesha vifaa vyao wenyewe vya kuhifadhia bidhaa hizo? Linganisha mawazo yako na mapendekezo yaliyopo katika Nyenzo Rejea 3 .
Somo la 3
Kusoma na kuandika kunaweza kusisimua na kuchangamsha sana, lakini baadhi ya wanafunzi wanajenga mtizamo hasi kuhusiana na shughuli hizi. Sababu inaweza kuwa ni kwa vile wanagundua kuwa kusoma na kuandika ni kugumu, labda kwa sababu wanaweza kuchoshwa na kazi za usomaji na uandishi ambazo zinafuata ruwaza zilezile daima, au labda hawaoni thamani kubwa katika usomaji na uandishi. Moja ya changamoto zako kama mwalimu ni kuamsha ari ya wanafunzi katika usomaji na uandishi na kuwafanya wahamasike.
Uchunguzi Kifani 3 na Shughuli Muhimu vinapendekeza shughuli ambazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi wafurahie na wajiamini zaidi katika usomaji na uandishi.
Uchunguzi kifani ya 3: Kusoma alama zinazopakana jirani na eneo lako na kuandika maelezo kuhusiana na alama hizo
Bwana Richard Limbunga hufundisha Kiswahili Darasa la 5 jijini Dar es Salaam. Dar es Salaam ni eneo lenye watu wengi na mifano mingi ya chapa za kimazingira kuzunguka shule –mifano mingi zaidi ni ya Kiswahili lakini pia kuna mifano kutoka katika lugha mbalimbali za asili.
Ili kuongeza kipato watu wameanzisha ‘biashara za uani’ kama vile maduka ya bidhaa ndogondogo za dukani, sehemu za kunyolea, warepeaji magari na vibanda vya simu. Sehemu zote hizi zina alama na baadhi pia zina matangazo ya kibiashara kwa ajili ya bidhaa mbalimbali. Hizi ni shule, kliniki, sehemu na kumbi za kuabudia, ambazo nyingi yazo zina alama na mbao za matangazo. Katika barabara kuu, kuna alama sehemu nyingi, zikiwemo Chuo Kikuu maarufu cha Dar es Salaam.
Bwana Limbunga alipanga safari kuzunguka Dar es Salaam ambayo ingewapatia wanafunzi fursa ya kusoma na kutengeneza kitini na michoro kuhusu mifano mbalimbali ya chapa na maumbo yanayoonekana. Pia aliandaa orodha ya maswali ili kuongozo uchunguzi wao.
Bwana Limbunga anao wanafunzi 58 katika darasa lake, wakiwemo kumi ambao wamewasili hivi karibuni kutoka Burundi. Aliamua kuwaomba wastaafu wawili wanaojua lugha nyingi wamsaidie katika shughuli hii. Mmoja anaongea Kirundi, lugha ya wanafunzi kutoka Burundi. Vikundi vitatu vya darasa lile vilikwenda safari.
Marafiki wa Bwana Limbunga walishiriki katika mjadala darasani na kwenye shughuli zilizofuata za usomaji na uandishi. Kufikia mwishoni mwa wiki, watu wale watatu walikubali kuwa wanafunzi wamejua zaidi jinsi taarifa inavyoweza kuwasilishwa kwa njia mbalimbali na kwa lugha mbalimbali na baadhi walionekana wamefurahia zaidi usomaji na uandishi kuliko hapo awali.
Shughuli muhimu: Kusoma Alama
Kabla ya somo, soma Nyenzo Rejea 4: Kujiandaa kwa matembezi ya kijumuiya ili kupanga matembezi na kuandaa maswali yako. Andika maswali ubaoni.
Ili kuanza somo, waambie wanafunzi kuhusu matembezi na, kama wanaweza, waambie wanakili yale maswali kutoka kwenye ubao. Kama hawawezi, andaa orodha ya maswali kwa kila kiongozi wa kikundi kwa ajili ya kuwauliza katika matembezi.
Wachukue kwa ajili ya matembezi yaliyopangwa mpaka kwenye jumuiya yenu mnayokaa.
Wakiwa wanatembea, lazima watoe au waandike majibu ya maswali na wachore mifano ya chapa au picha wanazoziona.
Baada ya muda, waambie wanafunzi kwenye vikundi washirikishane kile walichokiona, walichokiandika na walichokichora. Liambie darasa zima liripoti na lirekodi pointi muhimu ubaoni.
Kiambie kila kikundi kichore, kiandike jina na kichore alama, ilani au tangazo wanalofikiri ni muhimu kuwapo katika jumuiya zao. Wasaidie katika maneno yoyote magumu. Watoto wadogo wanaweza kuhitaji kufanya kazi kwenye vikundi vidogo vyenye mtu mzima wa kuwasaidia.
Kiambie kila kikundi kioneshe mchoro wao darasani kisha kieleze uteuzi wa lugha, maumbo na taarifa.
Onesha michoro hii darasani ili wanafunzi wote waisome.