SHAIRI: NAKUPENDA ABDUL - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NAKUPENDA ABDUL (/showthread.php?tid=685) |
SHAIRI: NAKUPENDA ABDUL - MwlMaeda - 07-31-2021 ABDUL Ingelikuwa ni vazi, nivue nivae hili, Ningesema waziwazi, nivalishwe Mara mbili, Ujue natokwa chozi, nikuwazapo rijali, Nakupenda Abdul, mfanowe sielezi. Huyu tumetoka mbali, tangu Ile mwakajuzi, Nimeshaona dalili, bila wewe sijiwezi, Japo tungali awali, moyo wangu hausizi, Mfanowe sielezi, nakupenda ABDUL. Mara hunitoka chozi, nikulilie wa mbali, Pengine ninajihizi, najona Kama tumbili, Na hisi zangu za mwili, kwingineko haziwazi, Nakupenda ABDUL, mfanowe sielezi. Sasa yapita miezi, wanahari walaili, Unadhani sikuwazi, ati nimuwaze Ally, Nakumbuka mwaka juzi, unipe lile na hili, Nakupenda ABDUL, mfanowe sielezi. Nile wali la ugali, kwa nini huniulizi, Kachumbari na kachori, au mboga chainizi, Najiuliza maswali, kwa nini huniulizi? Mfanowe sielezi, nakupenda ABDUL. Sasa nimekuwa chizi, ujue silali sili, Nilalavyo macho wazi, niwaze ulivyo mbali, Unahama usingizi, nihurumie rijali, Nakupenda Abdul, mfanowe sielezi. Kama Mzee Mpili, nilivyoishiwa pozi, Yanga wapo kosa goli, wabubujikwe machozi, Kwangu imezidi hali, niokoe sijiwezi, Nakupenda ABDUL, mfanowe sielezi. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 RE: SHAIRI: NAKUPENDA ABDUL - MwlMaeda - 08-01-2021 Mwili umepata ganzi,kinywa nacho cha chatetema Kwa hayo yako mapenzi, Napata tabu kuhema Niweke wazi mtunzi,hili penzi toka zama? Filieda sema kweli,sinipandishe mzuka Unachokinena kweli,ama utani waleta? Uidhuru yangu hali,kwako pindi kijileta Bainisha tafadhali,lifumbue fumbo tata Filieda sema kweli,sinipandishe mzuka Penzi lako kama jipu,limechipua ghafula Lisijekua upupu,niwashwe nishindwelala Kumbe ni porojo tupu,nife nizikwe Mbagala Filieda sema kweli,sinipandishe mzuka Tamati mwisho nafika,nakifariki kikao Mno nimehamasika,ngoma yataka matao Koti likikosa shati huwa kama kuzubao Filieda sema kweli,sinipandishe mzuka Mwl Abdul Ndembo(Wingu zitu) Mburahati sekondari-0717573661 |