KAULI -TAURIA/VITANZA NDIMI NA MICHEZO YA MANENO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: KAULI -TAURIA/VITANZA NDIMI NA MICHEZO YA MANENO (/showthread.php?tid=673) |
KAULI -TAURIA/VITANZA NDIMI NA MICHEZO YA MANENO - MwlMaeda - 07-30-2021 KAULI -TAURIA/VITANZA NDIMI NA MICHEZO YA MANENO Mara nyingi vitanza ndimi au wengine huita kauli tauria hutazamwa kuwa ni kitu kimoja na michezo ya maneno (Mulokozi, 1996; Wamitila, 2010). Mtazamo huu sio sahihi kwani kuna tofauti ya msingi kati ya kauli tauria au vitanza ndimi kwa upande mmoja, na mchezo wa maneno kwa upande mwingine (Okpewho, 1992). Vitanza ndimi au kauli tauria hurejelea maneno yenye mchanganyiko au mfuatano wa sauti zinazotatanisha kuzitamka kwa kasi pasipo kuzikosea. Hivyo basi, vitanza ndimi au kauli tauria hukusudiwa kuleta changamoto ya kimatamshi hasa mtu anapotakiwa kutamka maneno husika kwa kasi sana na ahakikishe anatamka pasipo kukosea. Kuna mifano kadhaa
katika Kiswahili inayohusiana na vitanza ndimi au kauli tauria. Mifano hiyo ni pamoja na hii ifuatayo: – Kale kakuku kikwekwe kapo kwako kaka?
– Mchicha mbichi mpishi mbishi, sichi hichi sichi sichi kikucha cha kuchi
– Kipi kikusikitishacho?
– Bili bought a bit of butter but a bit of butter was bit bitter so Bili bought a bit of butter again to make a bit of butter better.
– Katai is a masai, katai can tie and untie a tie, if katai can tie and untie a tie why can’t I tie and untie a tie like katai?
Kwa upande wa mchezo wa maneno, huhusisha mpangilio wa maneno ambayo huonekana kuwa na tahajia na hata matamshi ya namna moja lakini namna yanavyotumika yanaonesha kuwa na maana tofauti. Kuna baadhi ya michezo ya maneno inakuwa na namna fulani ya utatanishi katika matamshi kidogo. Hali hii haifanyi michezo hii ya maneno kuwa kauli tauria au vitanza ndimi. Mifano ya michezo ya maneno ni pamoja na hii iguatayo:
– Wale wali wale wali wao
– Katibu kata wa kata yam kata amekataa katakata
kukata miti katika kata yake. Kwa ujumla vitanza ndimi na kauli tauria hutumiwa sana katika michezo ya watoto na dhima kubwa zaidi katika jamii ni kufundisha watoto lugha hususani kipengele cha kimatamshi lakini pia kama burudani tu kwa watoto wakati wamejipumzisha. Michezo ya maneno licha ya kwamba pia hutumiwa na watoto kwa kiasi kingine katika jamii ya Waswahili hutumiwa sana hususani na washairi wa Kiswahili. Kwani kuna bahari mahususi ya ushairi wa Kiswahili inayojulikana kwa jina la zivindo. Bahari hii ni mahususi katika kufundisha lugha na imejikita sana katika matumizi ya mchezo wa maneno. Ufuatao ni mfano wa mchezo wa maneno kutoka katika ushairi wa zivindo: Kaa ni kusema kaa, na muwaliko ni kaa
Kaa ni alosimama, wamueleza kukaa
Kaa ni lililozima, na lilio moto ni kaa
Mwenye ya tano yafaa, anene ni kaa gani?
Kanda ni kanda mwili, uniondoe mavune
Kanda unga kwa samli, na maji yatangamane
Kanda tandika mahali, tupate keti tunene
Na la samaki ni lane, tena kuna kanda gani?
(Njogu na Chimera (1999)
|