MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NIKIWAZA KIFO CHANGU - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: NIKIWAZA KIFO CHANGU - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: NIKIWAZA KIFO CHANGU (/showthread.php?tid=638)

SHAIRI: NIKIWAZA KIFO CHANGU - MwlMaeda - 07-25-2021

SIJUI

Kuna muda peke yangu, nikiwa nimetuliya,
Ama niko na wenzangu, habari nawaambiya,
Ghafula mawazo chungu, jamani yananijiya,
Nakiwaza kifo changu, ni vipi kitatukiya?

Kwani ni wajibu kwangu, kuuka kwenye duniya,
Kurudi kwa Mola wangu, muda utapowadiya,
Nakiwaza kifo changu, ni vipi kitatukiya?

Sijui barabarani, nikiwa ninakimbiya,
Ama nikiwa shambani, mpunga napaliliya,
Au nikiwa chumbani, tuli nimejilaliya,
Nakiwaza kifo changu, ni vipi kitatukiya?

Wenda natoka kazini, katikati kwenye ndiya,
Wakatokea wahuni, kundi wakanivamiya,
Kupora vya mfukoni, na visu wakanitiya,
Nakiwaza kifo changu, ni vipi kitatukiya?

Sijui kwa kuugua, ikazorota afiya,
Tiba dafu zikafua, kila ninavyotumiya,
Maradhi nisoyajua, hatima nikafikiya,
Nakiwaza kifo changu, ni vipi kitatukiya?

Ama nikiwa garini, mimi nao abiriya,
Gari likapiga chini, na kuanza bingiriya,
Tama yangu masikini, hapo ndipo nikafiya,
Nakiwaza kifo changu, ni vipi kitatukiya?

Huwa nalikosa jibu, vipi nitatamatiya?
Hapo ndipo taratibu, kilio mie huliya,
Namlilia Mujibu, huku nikigugumiya,
Nakiwaza kifo changu, ni vipi kitatukiya?

Siwezi tena kusema, vigumu inaniwiya,
Mwili unanitetema, nguvu zimeniishiya,
Nijalie mwisho mwema, ninakuomba Jaliya,
Nakiwaza kifo changu, ni vipi kitatukiya?

Mshairi Machinga,
mfaumehamisi @gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.