ONYA = ONESHA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ONYA = ONESHA (/showthread.php?tid=612) |
ONYA = ONESHA - MwlMaeda - 07-22-2021 *ONYA = ONESHA* MBWENE! Mbwene shumndwa na mbuzi, wachandamana pamoya Na kuku mke na kozi, wana wao wachileya Na mtu msi maozi, *akionya* watu ndiya Hayano sikusikiya, niwene kwa mato yangu! - _Diwani ya Muyaka bin Haji _(1940), uk. 66 Maana yake kwa nathari: Nimeona fisi na mbuzi, wakiandamana pamoja Na kuku jike na kozi,* wakilea watoto wao Na mtu asiye na macho (kipofu), *akionesha* watu njia Haya sikusikia, nimeona kwa macho yangu! *Kozi ni aina ya ndege afananaye na mwewe. Na hivi karibuni nilipokuwa nikiandikiana humu na mwenzetu, Bi Kawthar, kuhusu jambo jengine, niliunukuu wimbo huu maarufu uliotumiliwa neno "kuonya" kwa maana ya "kuonesha": U muongo, Basawera u muongo Kuna kijiti kimoja kikasimamisha jengo?, Huna pau huna mvinde huna ng'ongo, Nenda ukakate miti nije *nikuonye* jengo. - Abdilatif Abdalla Hamburg, Ujerumani 21 Julai, 2021 |