SHAIRI: NYOYO ZETU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NYOYO ZETU (/showthread.php?tid=603) |
SHAIRI: NYOYO ZETU - MwlMaeda - 07-20-2021 NYOYO ZETU Kwa moyo mie nakiri, Natamka kwa ulimi Nyota nimeitabiri, Nikawa sina usemi Bora nifichue siri, Ninayempenda mimi Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Macho hayakukosea, Yalipokuona wewe Na nafsi kungojea, Nikangiwa na kiwewe Huu wangu upokea, Moyo nakupa mwenyewe Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Zama za tokea enzi, Nilikupenda kwa dhati Moyo kujawa mapenzi, Kukupata ni bahati, Naeleza kwa utenzi, Maandishi yenye hati Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Waja wa kale wanena, Ya kweli usikatae Mahaba yenye kufana, Mpende akupendae Simfanyie khiyana, Moyo wake uutwae Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Penzi sitie ukungu, Sitochoka kukungoja Asali isiwe chungu, Wewe ndiwe namba moja Usinitie machungu, Moyo damu ukatoja Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Kila jambo la msingi, Ndani yake lina kheri Tutavikwepa vigingi, Tuepukane na shari Mahasidi kwetu wingi, Usinambie kwaheri Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Penzi la watu wawili, Kulipangua mashaka Nimeshapima akili, Kuamua nakutaka Nakupenda kikamili, Sitoitoa talaka Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Unikumbuke kwa huba, Usingizini na ndoto Tuitane mahabuba, Huku kipeana joto Ulojaliwa mahaba, Na mapenzi motomoto Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Wala sione aibu, Na kuniwacha njiani Unitibu nikutibu, La azizi u’mwandani Tulishane na zabibu, Tukiwepo kitandani Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Tamati nimeshafika, Namalizia shairi Nimechoka kuandika, Nimepungukwa na ari Nakupenda kwa hakika, Mpenzi usighairi Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida Na. TRT Swahili |