SHAIRI: IMPUZU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: IMPUZU (/showthread.php?tid=568) |
SHAIRI: IMPUZU - MwlMaeda - 07-15-2021 [attachment=410] IMPUZU. ------------ Jama nitoe utata, muache kusitasita, maswali mkiyaleta, kitwani yaliyokita, kuhusu vazi la jadi. ________ Kuhusu vazi la jadi, walipataje wa jadi, kitambaa siyo jadi, ya wahenga wetu jadi, vitu gani walivala? _________ Mababu na bibi zetu, wali na mbinu za kwetu, ngozi za wanyama wetu, magome ya miti yetu, vema yakiwasitiri, _________ Wali nao utambuzi, wa kutengeneza ngozi, magome walimaizi, miti kufanyia kazi, na mitindo wakavala. _________ Magome kwetu Ruanda, wahenga waliyapenda, Impuzu ni Kinyarwanda, ni nguo waliziunda, toka magome ya miti. _________ Makabila Tanzania, na Kenya ninawambia, Uganda, Burundi pia, Kongo na huko Zambia, impuzu walizivala. _________ Jadi yetu siyo siri, naionea fahari, ya kale nikivinjari, nipate wake uzuri, niupambe kwa shairi. _________ Rwaka rwa Kagarama, Mshairi Mnyarwanda, Wilaya ya Nyagatare, Jimbo la Mashariki,RWANDA. |