SHAIRI: KUSHINDANA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: KUSHINDANA (/showthread.php?tid=487) |
SHAIRI: KUSHINDANA - MwlMaeda - 07-10-2021 KUSHINDANA Mara nyingi kushindana kunayapoteza mambo, Kwaye bibi nae bwana, hadi yakaenda kombo, Hapafai! Mara nyingi kushindana, kunaharibu upendo, Wawili walopendana, wote wakachapa mwendo, Hapafai! Mara nyingi kushindana, ndiko huzua tatizi, Watu kutoelewana, wakashindwa fanya kazi, Hapafai! Mara nyingi kushindana, kunazua uchochezi, Uongo kusemeana, kazi ikawa telezi, Hapafai! Mara nyingi kushindana, ndiko huzua vihoja, Watu wakafarakana, ukapotea umoja, Hapafai! Mara nyingi kushindana, uzalisha matabaka, Hivyo ikashindikana, kufika wanapotaka, Hapafai! Tama waja kushindana, pawe penye manufaa, Kushindana kwa maana, kusikozua balaa, Panafaa! Mshairi Machinga, mfaumehamisi@gmail.com, +255716541703/752795964, Dar es salaam, Kkoo. |