SHAIRI: SIKIFUNUI KITABU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: SIKIFUNUI KITABU (/showthread.php?tid=476) |
SHAIRI: SIKIFUNUI KITABU - MwlMaeda - 07-09-2021 SIKIFUNUI KITABU Mie kijana labibu, ni lazima nichukue, Ziloweka taratibu, hilo jambo mn'gamue, Sikifunui kitabu, mpaka nikinunue. Sitaki wapa adhabu, wakutubi nisumbue, Walivyotunza vitabu, kurasa nivurugue, Sikifunui kitabu, mpaka nikinunue. Wala sijapanga tabu, unasi ilo mjue, Ila ni yangu adabu, naombeni mtambue, Sikifunui kitabu, mpaka nikinunue. Japo kwenu ni ajabu, mwaona maruerue, Watu wengi aghalabu, lazima wakifunue, Sikifunui kitabu, mpaka nikinunue. Ninazo nyingi sababu, zilofanya niamue, Ambazo ni mujarabu, niombeni mzijue, Sikifunui kitabu, mpaka nikinunue. Mosi hii ya mababu, "kiso chako sifungue" Nitazikosa sawabu, kwa mola nikaungue, Sikifunui kitabu, mpaka nikinunue. Hapa naishusha nibu, kikomo mie nitue, Ghulamu pia shaibu, kwangu hili mchungue, Sikifunui kitabu, mpaka nikinunue. Mshairi Machinga, mfaumehamisi@gmail.com, +255716541703/752795964, Dar es salaam, Kkoo. |