MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: BAJAJI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: BAJAJI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: BAJAJI (/showthread.php?tid=463)

SHAIRI: BAJAJI - MwlMaeda - 07-09-2021

[attachment=332]

BAJAJI

Naanzaje kusubiri, nisifike wanguwangu,
Nikajitesa sadiri, bure kujipa uchungu
Ikiwa mie tayari, nishaona jambo langu,
Mwanao nimeiona, bajaji ya ndoto zangu.

Siwezi kufanya ghuri, sinacho kiburi changu,
Bajaji hiyo nzuri, umbo lake kama dungu,
Inayokwenda vizuri, hitaji la moyo wangu,
Mwanao nimeiona, babaji ya ndoto zangu.

Mwenyewe nimedhihiri, sio bajaji ya tangu,
Umbo nayo matairi, bora hayana ukungu,
Yazidi hadi magari, ya warabu na wazungu,
Mwanao nimeiona, bajaji ya ndoto zangu.

Mama naona dhahiri, inashinda za wenzangu,
Ukiona utakiri, "umechagua mwanangu"
Wala haina kikiri, kupandwa na watu chungu,
Mwanao nimeiona, bajaji ya ndoto zangu.

Haiwezi niadhiri, naapa haki ya Mungu,
Bajaji naitabiri, nitapanda peke yangu,
Hawatopanda abiri, hata marafiki zangu,
Mwanao nimeiona, bajaji ya ndoto zangu.

Tamati hizi habari, umwambie na kakangu,
Nitazilipa dinari, bajaji iwe ya kwangu,
Kuwa nayo ni fahari, kuu maishani mwangu,
Mwanao nimeiona, bajaji ya ndoto zangu.

Mshairi Machinga,
mfaumehamisi@gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.