MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SHAIRI : NA TUZISOME SILABI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : NA TUZISOME SILABI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : NA TUZISOME SILABI (/showthread.php?tid=461)



SHAIRI : NA TUZISOME SILABI - MwlMaeda - 07-08-2021

NA TUZISOME SILABI
A-ndika herufi A, ikufae maishani,
E-ndelea kutambua, E herufi makini,
I-ndiyo hufwatia, mpango wa shairini,
O-na nivyo pangilia, ya nne mlolongoni,
U-some ukianzia, a e i o u kujua.


Ba-ada kuzitambua, zile herufi msingi,
Be-ba kitabu funua, uone silabi nyingi,
Bi-diisha kuzijua, usome mahali pengi,
Bo-ra ukazirudia, ndilo jambo la msingi,
Bu-re ukihudhuria, shule uchekwe na wengi.


Da-rasa mfano wake, DA inapotumika,
De- hufwata mbeleke, DA ukisha tamka,
Di- haina makeke, ya tatu kuitamka,
DO -kwenye dodo lake, tupate kuipachika,
DU- ya tano ushike, silabi isijetoka.


KA-ribu silabi KA, tusome na kuandika,
KE- katika mKEka, na Kenya pia tamka,
KI-jiko hiyo KI shika, uirukie haraka,
KO-koriko likiwika, jimbi tunapoamka,
KU- ni KUKU kumbuka, kukariri ukitaka.


SA-sa tufikie SA, silabi ja vile SAa,
SE-sa ndio neno hasa, SE silabi kujua,
SI-nikupe darasa, ya tatu kupangilia,
SO-ma uzijue sasa, na SO kuitambua,
Sungura mjanja hasa, SU hapo chungulia,


PA-pai lingali bichi, PA mwapopoa chini,
PE-ngine lisiwe bichi, ila rangi ya majani,
PI- jicho siPIkichi, eti nikaona soni,
PO-mfano wa pochi, PO ukaibaini,
PUu- natema simchi, PU silabi shikeni.


GA- silabi naanza, mufumbue masikio,
GE-pia nawafunza, pasipoweka kituo,
GI-usijejiponza, kuyaziba masikio,
GO-doro ninalitenza, silabi mjifunzio,
GU- ni ya tano anza, GA GE GI GO GU ujue.


YA- natuimbe yai, YA silabi nalenga,
Yeye hili halijui, mana angali mchanga,
YI mfano sijui, neon lake kulitunga,
YO-yo machozi silii, nyinyi mnione bunga,
Yule wala hafikii, utunzi wangu malenga.


NA-tuanze sasa NA, silabi kufurahie,
NE- nayo hufwatana, NA iifwatilie,
NI-nato hukazana, ya tatu ijishindie,
NO-mithili ya Nona, NO hapo ipigie,
NU-muache kanuna, hataki ajichekee.


RA-ngi za bendera yetu, ni nne zimetimia,
RE-ki ni muhimu kwetu, taka tukazizolee,
RI-silabi ya tatu, maRIngo hutumilia,
RO-ho ya mtu si kitu, ila anayowazia,
RU-di darasa na tatu, la nne hujazoea.


Usikae kama fyatu, suKWA nawe upendeze,
Ujuavyo sisi watu, SoKWE asizungumze,
Hawezi baki sukutu, KWIKWI litakuchomoze,
KWO sijapata kitu, OkonKWo nimueleze,
KWU huja kitututu, ya tano ajitimize.


LAleni nimebaini, kusoma mumeshachoka,
Leo siendi mbeleni, kituo hapa naweka,
LIle liwatatizeni, msiache litamka,
LOlote niambieni, naLO nitashughulika,
LULU kusoma jamani, ujinga tumeuzika.


Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704



RE: SHAIRI : NA TUZISOME SILABI - John John - 09-02-2021

Ahsante sana kwa kutukumbusha