SHAIRI: JIKO MAFIGA MATATU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: JIKO MAFIGA MATATU (/showthread.php?tid=307) |
SHAIRI: JIKO MAFIGA MATATU - MwlMaeda - 06-26-2021 JIKO MAFIGA MATATU Jiko ninalalamika, yangu haki siioni, Akili yanifumuka, jambo niwaambieni, Moja jifya kuinjika, salama iwe chunguni, Jiko MAFIGA matatu, iwaje nipewe moja? Leo haki ninataka, mawili tena nipeni, Moja limenipa Shaka, nifanyie kazi gani? Chungu kinateteleka, mwishowe kitue chini, Jiko MAFIGA matatu,iwaje nipewe moja. Sifa mumenitunuka, Moto nawapatieni, Kimoja ninachotaka, yake MAFIGA pembeni, Kuni zikiongezeka, mtanijaza jubuni, Jiko MAFIGA matatu, iwaje nipewe moja? La kwanza jifya nataka, ukubwawe wastani, Chungu kikishachemka, kisitiwe mashakani, Hili jifya hukishika, mtindo wa kidizaini, Jiko MAFIGA matatu, iwaje nipewe moja? La pili nalitamka, liwe pana kumbukeni, Chungu ninapokiweka, kikaavyo kifasheni, La tatu kulipachika, wake upande wa tatu, Jiko MAFIGA matatu, iwaje nipewe moja? Jiko Sasa naondoka, hizi habari shikeni, Tena usipite mwaka,nitakalo litendeni, Msione ninawaka, moja jifya latoshani, Jiko MAFIGA matatu,iwaje nipewe moja? Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |