Jifunze Kiswahili cha kibiashara (Kiswahili kwa wageni) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Kiswahili kwa wageni (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=8) +--- Thread: Jifunze Kiswahili cha kibiashara (Kiswahili kwa wageni) (/showthread.php?tid=298) |
Jifunze Kiswahili cha kibiashara (Kiswahili kwa wageni) - MwlMaeda - 06-26-2021 Shopping, Buying and Selling
Business:
Shopping, Buying and Selling
[biashara: ununuzi, upigaji bei na uuzaji]
A). Business
MIFANO ZAIDI:
hazina [treasure]
hisa [shares]
hundi [draft; check; money order]
maafikiano [agreement]
malipo [pay (noun)]
mapatano [agreement]
mazao [produce (noun)]
mkopo [loan]
mnada [stock exchange]
dalali; mnadi [stockbroker]
taflisi [bankruptcy]
muflisi [bankrupt]
rasimali [natural resources]
malighafi [raw materials]
ujira [wage]
pesa taslimu [cash]
bwanyenye [capitalist]
mwinyi [lord]
akaunti ya akiba [savings account]
akaunti ya amana [deposit account]
akaunti ya hundi [checking account]
bidhaa muhimu [essential commodities]
haki halali [square deal]
hali ya uchumi [economic state]
hawala za serikali [treasury bills]
kuhodhi bidhaa [stockpiling]
mahitaji ya biashara [business stock]
mapatano ya biashara [transaction]
mpango wa biashara [business plan]
mwenye hisa [stockholder]
pigania bei [bargain (verb)]
soko la hisa [stock exchange]
B). Buying and Selling Vocabulary
bei [price]
ghali [expensive]
rahisi [cheap]
bei nafuu [fair price]
haipungui [does not reduce]
hakuna faida/maslahi [there is no profit]
ninataka [I want]
shilingi [shillings]
dola [dollars]
mwuzaji [shopkeeper]
mteja [customer]
Twende!
Twende dukani!
[Let’s go!]
[Let’s go to the store!]
pesa, hela [money]
Ghali sana! [Too expensive!]
Bei ghali! [The price is too high!]
punguza kidogo [reduce a little]
ongeza kidogo [add a little more]
bei rahisi sana! [very cheap price!]
Jamani, Mungu wangu!
C). International Currencies [Pesa za Kimataifa]
Pesa [Currency]
Dola [Dollar]
Taifa [Nationality]
Marekani / Kanada [U.S.A / Canada]
Pauni [Pound] Uingereza / Misri / Siria [Britain / Egypt / Syria]
Mak [Mark] Ujerumani [Germany]
Franki /
Faranga
[Franc] Ufaransa / Uswizi / Ubeljiji [France / Switzerland / Belgium]
Lira [Lira] Italia [Italy]
Yeni [Yen] Ujapani [Japan]
Krona [Króna] Uswidi/ Norwei [Sweden / Norway]
Schiling [Schilling] Austria [Austria]
Marka [Marka] Ufini [Finland]
Peseta [Peseta] Uhispania [Spain]
Rupia [Rupee] Bara Hindi [India]
Rand [Rand] Afrika Kusini [South Africa]
Shilingi [Shilling] Kenya / Uganda /Tanzania [Kenya / Uganda / Tanzania]
Birr [Birr] Uhabeshi [Ethiopia]
Kwacha [Kwacha] Zambia [Zambia]
Dinari [Dinar] Aljeria / Libya / Tunisia [Algeria / Libya / Tunisia]
Ougiya [Oguiya] Mauritania [Mauritania]
Dirham [Dirham] Mauritania [Mauritania]
Riale [Rial] Omani / Saudia [Oman / Saudi Arabia]
Sedi [Cedi] Ghana [Ghana]
Naira [Naira] Nigeria [Nigeria]
Yuro [Euro] Bara Ulaya [European Continent]
Zingatia [Note]
leta [bring]
nipe [give me]
nunua
uza
[buy] [sell]
ninataka [I want]
punguza [reduce; lower]
mteja [customer]
haipungui [does not reduce/lower]
vingi [a lot]
mbalimbali lipa mwuzaji [various] [pay] [shopkeeper]
Mazungumzo [dialogue]Kupiga bei [bargaining] Talking with a friend and going shopping for various items.
Halima: Hujambo Halima?
Anna: Sijambo. Habari za asubuhi?
Halima: Salama tu, nyumbani hawajambo?
Anna: Hawajambo.
Halima: Leo, unakwenda duka la vitabu / duka la dawa / duka la viatu / dukani /
sokoni kununua nini?
Anna: Ninakwenda kununua vitu / vichache / vidogo / vingi leo. Nitanunua
matunda / vyakula / vinywaji mbalimbali kama maembe, mapapai, na
machungwa. Wewe utanunua nini?
Halima: Mimi nitanunua vinywaji vichache vingi / vidogo / sana kama: soda,
pombe, maji ya machungwa, na divai. Pia nitanunua vifaa vya shule.
Anna: Haya, twende dukani sasa!
*At the shop/store* [dukani]
Mwuzaji : Karibu! Karibu!
Anna na Halima: Asante.
Mwuzaji: Habari za asubuhi / mchana / jioni / kutwa / Habari gani / Shikamoo?]
Anna na Halima: Salama sana.
Anna: Daftari hili bei gani / Daftari bei gani?
Mwuzaji: Shilingi ishirini.
Anna: Na kitabu bei gani / Kitabu bei gani?
Mwuzaji: Shilingi kumi na tisa.
Anna: Vipi, bei haipungui? Bei ghali sana! Tafadhali punguza!
Mwuzaji: Bei haipungui. Bei ni rahisi sana/hakuna maslahi/faida. Tafadhali
ongeza kidogo.
Anna: Ninataka / Nipe madaftari saba.
Mwuzaji: Vipi, hutaki kitabu?
Anna: Hapana. Leo sina pesa nyingi/sina pesa za kutosha/nyingi. Nina pesa kidogo
sana. Mimi ni maskini.
Mwuzaji: Hapana / La! Wewe ni tajiri. Una mali nyingi. Tafadhali ongeza bei.
Anna: Kalamu bei gani?
Mwuzaji: Shilingi kumi
Anna: Na rula bei gani? / Rula bei gani?
Mwuzaji: Shilingi ishirini na tano
Anna: Jamani mungu wangu! Acha bwana / mama. Haiwezekani / Vipi, bei
haipungui? Bei ghali sana.
Mwuzaji: Bei haipungui. Bei ni rahisi/hakuna maslahi/faida
Anna: Nipe / Ninataka kalamu tatu na rula nne.
Mwuzaji: Sawa. Tafadhali leta pesa?
Anna: Sawa!
Mwuzaji: Utalipaje? Utatumia kedi / cheki / au pesa taslimu?
Anna:Nitatumia pesa taslimu. Akaunti yangu haina pesa.
Mwuzaji:Sawa. Hamna shida. Tafadhali leta kedi.
Anna: Ndiyo hii.
Mwuzaji: Asante sana. Kwaheri, wewe ni mteja mzuri. Rudi tena. Tutaonana wiki
kesho.
Anna: Kwaheri.
Mwuzaji: Kwaheri. Tutaonana baadaye. Inshallah.
Anna: (You can continue the same dialogue with Anna buying fruits, drinks, spices,
and foods by substituting them with the school items above).
|