Matumizi ya kihusishi "kwa" - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: Matumizi ya kihusishi "kwa" (/showthread.php?tid=2856) |
Matumizi ya kihusishi "kwa" - MwlMaeda - 11-02-2022 Matumizi ya kihusishi "kwa" 1. Huonesha mahali au upande: Mano, amekwenda kwa mjomba wake. 2. Huonesha sababu au kisababishi cha jambo: mfano; ninaishi kwa ajili yako. 3. Huonesha wakati: mfano; sina nafasi kwa sasa. 4. Huonesha sehemu Tulani ya kitu kikubwa, mfano: Mpira umekwisha wakiwa wamefungana nneĀ kwa tatu. 5. Huonesha jinsi kitendo kilivyotendeka: Mfano; alimvuta kwa nguvu sana ndio maana limevunjika. 6. Kuonesha matumizi ya kitu. Mfano: Alisafiri kwa basi |