MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Vitenzi vya Silabi Moja - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
Vitenzi vya Silabi Moja - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9)
+--- Thread: Vitenzi vya Silabi Moja (/showthread.php?tid=2852)

Vitenzi vya Silabi Moja - MwlMaeda - 10-27-2022

Vitenzi vya Silabi Moja
Hivi ni vitenzi vyenye silabi moja pekee. Ili kuleta maana kamili, vitenzi hivi huambatanishwa na kiungo KU- katika kauli ya kutenda. Kama vitenzi vingine, vitenzi vya silabi moja vinaweza kunyambuliwa. k.m: soma, kula, sikiza
  1. -cha - kucha - jua linapochomoza asubuhi k.m kumekucha

  2. -fa - kufa - kuacha kupumua, kupoteza uhai k.m amekufa

  3. -ja- kuja - fika mahali hapa k.m nimekuja

  4. -la- kula - kutia chakula mdomoni k.m anakula

  5. -nya- kunya - kutoa mabaki ya chakula toka tumboni k.m mtoto amekunya

  6. -nywa- kunywa - kutia kinywaji kama vile maji au maziwa mdomoni k.m ninakunywa uji

  7. -pa- kupa - kumkabithi/kumpatia mtu kitu k.m amenipa pesa

  8. -pwa- kupwa - kujaa hadi pomoni - k.m kisima kimekupwa maji

  9. -twa- kutwa - jua linapozama magharibi na usiku kuingia k.m kumekutwa

  10. -wa- kuwa - kutokea katika hali au mahali fulani k.m alikuwa