MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SANAA YA MAIGIZO - Printable Version
|
SANAA YA MAIGIZO - Printable Version
+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Sekondari (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=4)
+---- Forum: Kidato cha tano na sita (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=44)
+----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=45)
+----- Thread: SANAA YA MAIGIZO (/showthread.php?tid=285)
|
SANAA YA MAIGIZO - MwlMaeda - 06-26-2021
Maigizo ni sanaa katika fasihi simulizi ambayo watendaji huwa ndio wahusika. Maigizo hayasimuliwi kama mbinu nyingine za fasihi. Wahusika ndio huzungumza katika sehemu zao mbalimbali.
Mifano:
- Michezo ya Kuigiza (Jukwaani) – Haya ni maigizo ya jukwaani ambapo watendaji huiga maneno na matendo ya wahusika mbele ya hadhira.
- Miviga – Miviga ni sherehe mbalimbali katika jamii fulani. Watu hujumukika na sherehe hizi kulingana na tamaduni zao
- Ngomezi – ni sanaa ya ngoma. Midundo mbalimbali ya ngoma hutumika kuwasilisha ujumbe mbalimbali.
- Malumbano ya Utani – Malumbano ya utani ni mashindano ya kuongea jukwaani baina ya watu wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku kukejeli tabia mbaya katika jamii au kundi fulani
- Ulumbi – Ulumbi ni uwezo wa kipekee wa kuzungumza mbele ya hadhira. Mtu mwenye uwezo huo wa kipekee wa kuzungumza jukwaani huitwa mlumbi.
- Soga – Soga ni mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu huwa hayana mada maalum.
- Vichekesho – Vichekesho ni aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa vihadithi vifupi au sentensi zenye uwezo wa kuwafanya wasikilizaji wacheke.
- Maonyesho ya Sanaa – Maonyesho huhusisha watu wa jamii au kundi fulani wanaoonyesha taaluma, ujuzi au sanaa yao kwa watazamaji.
RE: SANAA YA MAIGIZO - MwlMlela - 06-28-2021
Kwa majibu haya, nimefanikiwa kujua tofauti ya maigizo na sanaa za maonesho.
|