ETIMOLOJIA YA NENO "DAHALIA'' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "DAHALIA'' (/showthread.php?tid=2842) |
ETIMOLOJIA YA NENO "DAHALIA'' - MwlMaeda - 10-12-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "DAHALIA'' Neno *dahalia* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo: 1. Jengo wanamolala wanafunzi wasomao kwenye shule au vyuo vya bweni *(Kamusi Kuu ya Kiswahili*). 2. Bweni la wanafunzi wa kike.( *Kamusi Teule ya Kiswahili*). Neno hili *dahalia* linatokana na neno la Kiarabu *daakhiliyyat داخلية* lenye maana zifuatazo: 1. Shule ya bweni, *madrasatun Daakhiliyyat مدرسة داخلية.* 2. Kivumishi *-a ndani*, *mushkilatun daakhiliyyat مشكلة داخلية* tatizo la ndani, *malaabisun daakhiliyyat ملابس داخلية* nguo za ndani, *wizaaratun daakhiliyyat وزارة داخلية* wizara ya mambo ya ndani. Kinachodhihiri ni kuwa neno *daakhiliyyat داخلية* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *dahalia* maana yake ya bweni katika lugha ya asili - Kiarabu (cha zamani) haikubadilika. Neno la Kiarabu Sanifu linalotumika kwa maana ya bweni ni *mahjau مهجع (umoja) na mahaajiu مهاجع (wingi).* *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |