MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO "DAFTARI'' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO "DAFTARI'' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "DAFTARI'' (/showthread.php?tid=2840)

ETIMOLOJIA YA NENO "DAFTARI'' - MwlMaeda - 10-08-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "DAFTARI''

Neno *daftari* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: li-/ya-*] yenye maana zifuatazo:

1. Kitabu kinachotumiwa na wanafunzi kuandikia masomo ya darasani na kufanyia mazoezi  *(Kamusi Kuu ya Kiswahili*).

2. Kitabu cha kutunzia kumbukumbu za miamala ya kifedha; leja.( *Kamusi Kuu ya Kiswahili*).

Neno hili *daftari* linatokana na neno la Kiarabu *daftarun  دفتر*  lenye maana zifuatazo:

1.  Karatasi zilizofungwa pamoja ambazo wanafunzi huandikia masomo yao darasani kama vile hesabati na kadhalika.

2. Daftari la kumbukumbu kwa ajili ya kuandikia matukio, fikra muhimu na kadhalika.

3. Kitabu cha hundi za benki,  brosha.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *daftarun دفتر* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *daftari* maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu  hazikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*