ETIMOLOJIA YA NENO "DAFRAO'' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "DAFRAO'' (/showthread.php?tid=2838) |
ETIMOLOJIA YA NENO "DAFRAO'' - MwlMaeda - 09-28-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "DAFRAO'' Neno *dafrao* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo: 1. Tukio la kugongana uso kwa uso kwa vyombo vinavyotembea. 2. Chuma kigumu kinachofungwa Mbele ya gari ili kuzuia uharibifu wakati magari yanapogongana. Neno hili *dafrao* linatokana na neno la Kiarabu *dafraau دفراء* na lenye maana zifuatazo: 1. Kilichodhalilika. 2. Kitu kilichooza, kikanuka na kutoa wadudu. 3. Aina ya mmea wa kitropiki. Kwa Kiingereza huitwa *scoparia.* Kinachodhihiri ni kuwa neno *dafraau دفراء* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *dafrao* maana yake kati lugha ya asili - Kiarabu ilibadilika na kupata maana mpya zilizotajwa. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |