ETIMOLOJIA YA NENO "BUGHUDHA'' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "BUGHUDHA'' (/showthread.php?tid=2809) |
ETIMOLOJIA YA NENO "BUGHUDHA'' - MwlMaeda - 08-23-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BUGHUDHA'' Neno bughudha katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya mambo yanayomkasirisha au kumuudhi mtu, maneno na vitendo vinavyomfanya mtu audhike. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili bughudha linatokana na tendo-jina la Karabu bugh-dhwun بغض lenye maana ya chuki linalotokana na kitenzi cha Kiarabu baghadhwa (soma: baghadhwa/yabghadhwu/bugh-dhwan بغض، يبغض، بغضا) chenye maana zifuatazo: 1. Kuchukia. 2. Kuchukiza. 3. Kuchukiwa. Kinachodhihiri ni kuwa neno bugh-dhwun بغض lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno bughudha lilichukua maana mpya ya maneno na vitendo vinavyomfanya mtu audhike, mambo yanayomkasirisha au kumuudhi mtu. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |