MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: CHOZI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: CHOZI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: CHOZI (/showthread.php?tid=2808)

SHAIRI: CHOZI - MwlMaeda - 08-23-2022

CHOZI
Alipokuwa kufani, pumzi ikimkwama,
Aliniita pembeni, maneno akiyasema,
Sijitie kilioni, machozi ukayafuma,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Hata ukilia sana, useme olele mama,
Bure wajitesa mwana, tatizole litakwama,
Kisha macho yatatuna, aibu kujitazama,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Useme uvue nguo, ukaanza kulalama,
Wala hupati funguo, tatizo kuliandama,
Hakina kitu kilio, wajongezea dhahama,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Kwa tatizo yake dawa, uanze kulisakama,
Mwishowe kulitatatua, kwa busara na hekima,
Wako moyo utapowa, furaha ukiifuma,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Wakati tukifiliwa, mfano baba na mama,
Moyo hutaki kutuwa, machozi hujaa pima,
Vipi wanafufuliwa? mwisho vichwa vyatuuma,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Tupatapo mitihani, ya mabonde na milima,
Mikono huwa kichwani, tulie olele mama,
Mwisho tunapata Soni, kulia mtu mzima,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Nilikuwa bado kinda, alipofariki mama,
Kilio sikukishinda, nililia Kama kinda,
Huku kule nilikwenda, yani aamke mama,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Chozi halikubadili, kwa punje au alama,
Sikuziona dalili, aamke wangu mama,
Ndipo likumbuka mbali, maneno aliyosema,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Siku niliyoamini, chozi halina salama,
Yangu hapo sithamini, kulivisha koja jema,
Machozi ni kitu duni, aminj ninayosema,.
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Kwa heri wanazuoni, ndugu zangu maulama,
Nimefika ukingoni, ndiyo yangu kaditama,
Kulialia ya nini, bure kujitia homa?
Halina thamani chozi, aliniusia mama.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704