ETIMOLOJIA YA NENO "BUDI'' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "BUDI'' (/showthread.php?tid=2806) |
ETIMOLOJIA YA NENO "BUDI'' - MwlMaeda - 08-21-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BUDI'' Neno budi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo: 1. Jambo la lazima. Msemo: Sina budi kusafiri: lazima nisafiri. (Kamusi Kuu ya Kiswahili). 2. Suala linalomlazimu mtu kulitimiza. Msemo: Sina budi kuwasilisha mada yangu leo. (Kamusi ya Karne ya 21) 3. Nomino (Msemo) Sina budi kuja kesho: Lazima nitakuja kesho; Hapana budi : lazima. (Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI). Katika lugha ya Kiarabu, neno hili budi linatokana na neno la Kiarabu buddun (soma: buddun/buddan/buddin بد) lenye maana zifuatazo: 1. Sehemu ya kitu, mbadala, kutengana. Waarabu hulitumia neno hili pamoja na herufi laa (لا), yaani: Laa budda لا بد kwa maana ya: hakuna mbadala, hakuna hiari, hakuna pa kukimbilia. 2. Sanamu, nyumba ya kuhifadhi sanamu. Kinachodhihiri ni kuwa neno buddun بد lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno budi lilichukua maana ya Laa budda inayoashiria 'ulazima' katika Kiarabu lakini wakalipa neno lenyewe ' budi ' maana ya 'lazima' ambayo ikitanguliwa na neno ' hapana ' linaleta maana kinyume na kilichokusudiwa. Neno ' budi ' lilipaswa kupewa maana ya hiari au kitu mbadala ili linapotanguliwa na neno ' hapana/sina' lilete maana ya ulazima. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |