ETIMOLOJIA YA NENO SHUKURANI '' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO SHUKURANI '' (/showthread.php?tid=2800) |
ETIMOLOJIA YA NENO SHUKURANI '' - MwlMaeda - 08-06-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO SHUKURANI '' Neno *shukurani* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya maneno yanayotolewa kuonesha kuupokea kwa mikono miwili wema uliotendewa; *ahsante/asante.* *Nahau* : *Toa shukurani:* sema ahsante. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *shukurani* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'shukraan* *(soma: shukraanun/shukraanan/shukraanin شكران)** tendo-jina *Masdar مصدر* la *kitenzi* cha Kiarabu *shakara شكر* chenye maana zifuatazo: 1. Amemsifu na kumtaja mtu mwengine kwa wema kutokana na hisani aliyomfanyia. 2. Amemlipa mtu mwengine malipo fulani kwa kuifanya vizuri kazi aliyomtuma. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *'shukraanun شكران* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *shukurani* halikubadili maana katika lugha ya Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |