MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BIASHARA' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'BIASHARA' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BIASHARA' (/showthread.php?tid=2799)

ETIMOLOJIA YA NENO 'BIASHARA' - MwlMaeda - 08-05-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BIASHARA'

Neno *biashara* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya mchakato wa kununua na kuuza mali au vitu.
*Biashara sukutu*: aina ya uuzaji na ununuaji wa bidhaa bila maongezi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *biashara* limechukuliwa kutoka maneno mawili ya  Kiarabu  *'bay-un* *(soma: bay-un/bay-an/bay-in  بيع)**  na *'shiraau* *(soma: shiraaun/shiraa-an/shiraain    شراء)**  yenye maana zifuatazo:
*Bay-un* ni:
1. Tendo-jina *Masdar مصدر* ya kitenzi cha Kiarabu *baa-a  باع* chenye maana ya *ameuza* .

2. Kitendo cha kuchukua kitu na kulipa thamani yake.

3. Kitendo cha kutoa kitu na kuchukua thamani yake.

4. Bidhaa za kuuzwa. 

Na *shiraau  شراء* ni:

1. Kitendo cha kutaka kununua kitu na kulipa thamani yake.

2. Mahali pa kuuza na kununua; *suuq سوق*, *soko* .

Kinachodhihiri ni kuwa maneno mawili ya Kiarabu *'bay-un wa shiraa بيع و شراء* yalipoingia katika Kiswahili na yalitoholewa kuwa neno *biashara* na neno hili la Kiswahili halikubadili maana ya msingi ya maneno hayo ya Kiarabu, kuuza na kununua.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*