ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHASHA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHASHA' (/showthread.php?tid=2784) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHASHA' - MwlMaeda - 07-18-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHASHA' Neno *bashasha* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo: 1. Hali ya kuonesha furaha; ucheshi, uchangamfu. 2. Furaha na uchangamfu. *Mfano:* Mgeni rasmi alipokelewa kwa bashasha kubwa. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bashasha* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'bashaasha* *(soma: bashaashatun/bashaashatan/bashaashatin بشاشة)** lenye maana zifuatazo: 1. Tendo-jina *masdar مصدر* la kitenzi cha Kiarabu *bash-sha بش* chenye maana ya: *amekunjua uso wake, amemfurahikia aliyekutana naye, amempa faraja.* 2. Hali ya kumlaki mtu kwa furaha na kicheko. 3. Uso mkunjufu uliojaa furaha na tabasamu. Kinachodhihiri ni kuwa neno *'bashaashatun بشاشة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bashasha* halikubadili maana yake katika lugha asili- Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |