MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAHARI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAHARI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BAHARI' (/showthread.php?tid=2679)

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAHARI' - MwlMaeda - 07-08-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAHARI'

Neno *bahari* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Sehemu ya maji chumvi yanayozunguka mabara na visiwa.

2. Kitu, eneo au jambo kubwa na lenye mawanda mapana.

*Msemo:* Elimu ni bahari: Elimu haina mwisho.

3. Mojawapo ya tungo za ushairi.

4. Mshororo wa mwisho wa ubeti usiobadilika katika kila ubeti wa shairi au utenzi.

5. Kitu kikubwa na kipana.
Msemo: Ana bahari ya shamba.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bahari* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'bahru* *(soma: bahrun/bahran/bahrin  بحر)** yenye maana zifuatazo:

1. Maji mengi yanayochukuliwa na mawimbi hadi nchi kavu, mfano Bahari Hindi.

2. Aina za tungo za mashairi au tenzi zipatazo 16 katika Arudhi ya Kiarabu.

3. Sehemu ya wiki, mwezi au mwaka.

4. Mawingu meupe mepesi ambayo hutanda kabla ya majira ya kiangazi.

5. Ugonjwa wa Kifua Kikuu unaosababisha kiu kikali na kuhitaji sana kunywa maji.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'bahrun بحر* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bahari* halikubadili maana yake inayohusu maji na aina ya tungo za ushairi katika lugha  asili ya Kiarabu bali liliongeza maana mpya ya ushairi ya mshororo wa mwisho wa ubeti usiobadilika katika kila ubeti wa shairi au utenzi.

*TANBIHI:*
Katika Arudhi ya Kiarabu neno *bahru (wingi: buhuurun)* lina maana ya aina za tungo za ushairi 16 nazo ni: AT-TWAWILU, AL-MADIIDU,AL-BASIITWU, AL-WAAFIRU, AL-KAAMILU, AL-HAZAJU, AR-RAJAZU, AR-RAMALU, AS-SARII-U, AL-MUNSARIHU, AL-KHAFIIFU, AL-MUDHWAARI-U, AL-MUQTADHWABU, AL-MUJTATHU, AL-MUTAQAARIBU NA ALMUHDATHU.
Mgunduzi wa bahari 15 ni AL-KHALILU BIN AHMAD AL-FARAAHIIDY na bahari ya 16 ambayo imeitwa AL-MUHDATH imeongezwa na mwanafunzi wake AL-AKHFASHU AL-AWSATWU.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*