MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAKAA' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAKAA' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BAKAA' (/showthread.php?tid=2634)

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAKAA' - MwlMaeda - 06-30-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAKAA'

Neno bakaa katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: li-/ya-, wingi: mabakaa] yenye maana zifuatazo:

1. Salio linalobaki baada ya matumizi ya kitu.

2. Kiasi cha fedha kinachobaki baada ya matumizi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili bakaa limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  'baqaa( soma: baqaaun/baqaa-an/baqaain بقاء ) ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Kukaa mahali, kudumu.

2. Kuendelea na jambo.

3. Kukaa milele, daarul baqaai دار البقاء nyumba ya milele; kuzimu.

4. Tendo-jina la kitenzi cha Kiarabu baqiya بقي chenye maana ya kudumu, kilichothibiti, kilichobakia kutokana na kitu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno 'baqaaun بقاء lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno bakaa lilichukua kutoka lugha ya asili - Kiarabu maana ya kilichobakia kutokana na kitu na likapewa maana ya salio linalobaki baada ya matumizi ya kitu, kiasi cha fedha kinachobaki baada ya matumizi.

TANBIHI:
Katika Kiarabu neno linalotumiwa kwa maana ya salio linalobaki baada ya matumizi ya kitu, kiasi cha fedha kinachobaki baada ya matumizi ni neno raswiid (soma: raswiidun/raswiidan/raswiidin رصيد).

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.