ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI' (/showthread.php?tid=2600) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI' - MwlMaeda - 06-15-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI' Neno *baathi* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Bath.i* [Kitenzi elekezi] chenye maana ya 'rejesha uhai wa mtu au kiumbe aliyekuwa amekufa; fufua. *Kisawe* : huisha. *Minyambuliko:* baathia, baathika, baathiwa, baathisha. 2. *Bath.i* [Kitenzi elekezi] chenye maana ya -pa mtu uwezo na mamlaka ya kwenda kufanya kazi au jambo kwa niaba ya mtu mwengine. 3. *Nomino [Ngeli:-a/-wa]* yenye maana ya kiongozi wa dini; mtume. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *baathi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'ba-aath*( *soma: ba-athun/ba-athan/ba-athin بعث )* ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Kufufua, kufufuliwa, kuhuisha *yawmul ba-athi يوم البعث* siku ya Kiyama. 2. Mtume, mitume. 3. Kumuamsha mtu toka usingizini. 4. Kikundi cha askari wapiganaji; jeshi. 5. Mtu asiyeweza kupata usingizi kutokana mazonge aliyokuwa nayo. 6. Furaha, utulivu. Kinachodhihiri ni kuwa neno *'ba-athun بعث* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *baathi* lilichukua baadhi ya maana kutoka Kiarabu na kuziacha zingine. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |