MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SHAIRI: KUJUWA NI MATATIZO - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: KUJUWA NI MATATIZO - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: KUJUWA NI MATATIZO (/showthread.php?tid=2598)



SHAIRI: KUJUWA NI MATATIZO - MwlMaeda - 06-13-2022

                  KUJUWA NI MATATIZO
 
            Lugha yangu ya asili, niijuavyo si haba, najivuniayo sana
            Lakini hii ya pili, ni Kizungu chanikaba, uwelevu nayo sina
            Ndipo juzi Jumapili, akanitanza swahiba, tukaanza kuvutana
            Aliniambia: Silly!, nikadhani anshiba, kumbe yuwanitukana!
 
            Kuelewa ni kuzuri, hukukinga na kujuta, ukawa hutazozana
            Hukupunguza kiburi, ukadharau kuteta, ukapenda kushikana
            Ja vile kaka Saburi, alivyonitia tata, mpaka nikadangana
            Na nilipomshauri, aliponambia: Better, hapo hapo nikakona
 
            Si mjinga kama gude, huzitumia fikira, nawambia muelewe
            Bao latezwa kwa ndude, na kazi ni za majira, yakupasa uyajuwe
            Nenda skuli 'sidode, ujinga una izara, yasikufike na wewe
            Naliambwa: Hey dude!, nikajibu kwa hasira:, Na wewe dude mwenyewe!
 
           Kujiweka nyumanyuma, jambo hilo likataye, usiwatwe mkiani
           Utafanyiwa hujuma, wenzako wakukimbiye, uulize: Kulikoni?
           Jana mimi nilikwama, nikasema nimwambiye, hanong'ona sikioni
           Akasema: Don't murmur, hasema: Mama nnaye, sijui wateka nini!
 
          Kimombo tulokikopa, kina sisi chatuuma, chatukutisha madhila
          Kisa hiki ningakupa, japokuwa chanitoma, kina funzo la sahala
          Sima twali twaichapa, akaingia Fatuma, akatuona tukila
          Akanita: Juma's papa, hamba: Papa si wa Juma, lakini waweza kula
 
 
         Mohamed Khamis.
         Takaungu, Kenya
          12.6.2022