MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'SWALA/SALA' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'SWALA/SALA' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'SWALA/SALA' (/showthread.php?tid=2593)

ETIMOLOJIA YA NENO 'SWALA/SALA' - MwlMaeda - 06-10-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'SWALA/SALA'

Neno *swala* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino:* yenye maana zifuatazo:

1. Ibada yenye mkusanyiko wa maneno na vitendo kama vile kukaa, kuinuka, kuinama, kusujudu pamoja na maombi ambayo ni moja ya nguzo tano za Uislamu.
   
2. Maombi ya msaada au kutoa Shukrani, yanayowasilishwa kwa Mwenyezi Mungu; dua.

3. Mnyama jamii ya tohe na kulungu anayeishi porini;  mnyama mwitu anayefanana na mbuzi.

Kwa maana ya ibada na maombi, kamusi za Kiswahili zimesajili pia matumizi ya neno 'sala'.

Neno *swala* katika lugha ya Kiswahili likitumika kwa maana ya ibada na maombi huwa ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] na likitumika kwa maana ya mnyama huwa ni huwa ni *nomino: [Ngeli: a-/wa-*].

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *swala/sala* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'swalaah*( *soma: swalaatun/swalaatan/swalaatin صلاة)* ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Maombi; dua.

2. Ibada mahsusi kwa Waislamu inayoanza kwa takbira (kusema: *Allaahu Akbar* ) na kumalizika kwa kutoa salamu (kusema: *Assalaamu Alaykum/Amani iwe juu yenu.*)

3. Rehema.

4. Nyumba ya ibada kwa Mayahudi.

5. Sifa njema, Tamko linalosisitiza upendo na udugu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'swalaah صلاة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *swala* lilichukua kutoka Kiarabu maana ya ibada na maombi, likabeba maana mpya ya mnyama mwitu anayefanana na mbuzi na kuziacha maana zingine katika lugha ya asili - Kiarabu.

*TANBIHI:*
Neno swalaah katika Uislamu lina maana tofauti kwa kuzingatia mtendaji: Swala kutoka kwa Mwenyezi Mungu ina maana ya rehema, kutoka kwa Malaika ina maana ya kuomba/kuombea msamaha na kutoka kwa binadamu na majini ina maana ya maombi.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

- - OlgaSano - 06-27-2022

Very remarkable topic