ETIMOLOJIA YA MANENO 'AKARABU/AKRABU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'AKARABU/AKRABU' (/showthread.php?tid=2588) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'AKARABU/AKRABU' - MwlMaeda - 06-04-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'AKARABU/AKRABU' Neno *akarabu* hutamkwa pia *akrabu* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* mshale katika uso wa saa unaoonyesha ama saa, dakika au sekunde. 2. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* mshale unaoonyesha uzito katika mizani. 3. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* mshale unaoonyesha upande fulani katika uso wa dira. Msemo: *Akarabu/Akrabu Kaskazini:* Upande wa Kaskazini. 4. *Nomino [Ngeli: i-/i-]* mkusanyiko wa nyota unaofanya umbo la *nge* angani. 5. *Nomino [Ngeli: i-/i-]* alama ya nge katika mfumo wa unajimu wa kutumia nyota. Katika lugha ya Kiarabu, neno *akarabu/akrabu* limekopwa kutoka nomino ya Kiarabu *aqarabun/aqaraban/aqarabin عقرب* yenye maana zifuatazo: 1. Mdudu mdogo mwenye sumu nyingi anayechoma kwa mwiba wa sumu ulio katika ncha ya mkia wake. 2. Moja ya nyota zilizo angani iliyo kati ya nyota za *Mizani* na *Mshale* na wakati wake unaanzia tarehe 24 Oktoba hadi tarehe 21 Novemba. 3. Aina ya samaki mwenye kichwa kikubwa ambaye hupatikana katika *Bahari ya Kati* (Bahari ya Mediteranea). 4. Mikanda ya viatu aina ya Kandambili. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *aqarabun/aqaraban/aqarabin عقرب* ) lilipokopwa na kutoholewa kuwa neno *akarabu/akrabu* lilichukua baadhi ya maana za lugha ya asili - Kiarabu na kuacha maana zingine na pia lilipata maana mpya ya upande *Akarabu/Akrabu Kaskazini:* Upande wa Kaskazini. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |