MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'TAMRINI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'TAMRINI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'TAMRINI' (/showthread.php?tid=2585)

ETIMOLOJIA YA NENO 'TAMRINI' - MwlMaeda - 06-01-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'TAMRINI'

Neno *tamrini*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Mazoezi yanayotolewa baada ya kufundisha somo fulani.

2. Jambo linalofanywa mara mwa mara na watu fulani kama kanuni; desturi, mwenendo.

Neno *tamrini* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *tamriinun/tamriinan/tamriinin تمرين* lenye maana zifuatazo:

1. Majaribio yanayotolewa baada kufundisha somo fulani kama vile lugha au hesabati.

2. Mazoezi ya viungo na ufundishaji mbinu mbalimbali za mchezo fulani  kwa lengo la kuimarisha mwili na kuuweka tayari. 

3. Mazoezi maalumu ya tasnia fulani kama vile mazoezi ya kijeshi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *tamriinun تمرين* lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *tamrini*  maana zake katika lugha asili - Kiarabu hazikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*