MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: MJA ANA SURA MBILI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: MJA ANA SURA MBILI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: SHAIRI: MJA ANA SURA MBILI (/showthread.php?tid=2576)

SHAIRI: MJA ANA SURA MBILI - MwlMaeda - 05-23-2022

MJA ANA SURA MBILI
Kuna maisha mawili, kwake mja duniani,
Kila aliye na mwili, haishi kama peponi,
Huwa ana sura mbili, malaika na shetani,
Ila twaiona moja, iwekwayo hadharani.

Hii sura ya awali, inapendeza machoni,
Lakini hii ya pili, wengine hawaioni,
Ingawa haiko mbali, kaiweka mafichoni,
Ila twaiona moja, iwekwayo hadharani.

Mwingine kutwa husali, anashinda ibadani,
Kuwa mja wa Jalali, kumbe toba! Mtihani,
Analo lile la pili, mfano kuwa muhuni,
Ila twaiona moja, iwekwayo hadharani.

Tungalijua ya pili, kuwa huyu ni shetani,
Tungetupilia mbali, kumtia masifuni,
Ila siye hatujali, kwa vile hatuioni,
Ila twaiona moja, iwekwayo hadharani.

Na wengine hawalali, watuchezea mwilini,
Kesho mavune ya mwili, hatujui kuna nini,
Kumbe yule mwanamwali, katufinyanga mwilini,
Ila twaiona moja, iwekwayo hadharani.

Ifichukapo ajali, ya pili kuibaini,
Tunaanza kujadili, na huyu eti jamani,
Yu vile tangu awali, alikuwa mafichoni,
Ila twaiona moja, iwekwayo hadharani.

Wala msinipe swali, ninatunga kuna nini,
Kwa wali na marijali, mja usimuamini,
Kesho taanguka chali, ukweli kiubaini,
Ila twaiona moja, iwekwayo hadharani.

Nafunga siendi mbali, usiku sasa laleni,
Nilosema muyajali, sijitie matatani,
kuna uongo na kweli,
Ila twaiona moja, iwekwayo hadharani.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704