ETIMOLOJIA YA NENO 'DHUKU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'DHUKU' (/showthread.php?tid=2572) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'DHUKU' - MwlMaeda - 05-20-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'DHUKU' Neno dhuk.u katika lugha ya Kiswahili ni kitenzi elekezi chenye maana ya onja ladha ya chakula, tia kitu mdomoni kwa ajili ya kujua ladha yake. Neno dhuk.u limechukuliwa kutoka kitenzi elekezi cha Kiarabu dhuq ( soma: dhuq/dhuuqi /dhuqaa/dhuuquu/dhuqna ذق ) kitenzi cha Kiarabu cha kuamrisha chenye maana ya onja ladha ya chakula au kinywaji. Kitenzi cha Kiarabu dhuq ذق (onja) kinatokana na kitenzi cha Kiarabu dhaaqa ذاق (ameonja) na maswdar مصدر (tendo-jina) dhawqu (soma: dhawqun/dhawqan/dhawqin ذوق) yenye maana zifuatazo: 1. Kuonja ladha ya chakula. 2. Kuonja adhabu; kuteseka. 3. Hisi zenye kuathiri zinazotokana na kazi ya kifasihi au kisanii. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu dhuq ذق lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno dhuku halikubadili maana yake katika lugha asili - Kiarabu. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |