ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUFU'' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUFU'' (/showthread.php?tid=2571) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUFU'' - MwlMaeda - 05-19-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUFU'' Neno arufu katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya nywele ndefu zinazoota kuzunguka shingo ya mnyama kama vile simba, farasi. Neno arufu limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu urfu ( soma: urfun/urfan /urfin عرف ) neno lenye maana zifuatazo: 1. Tabia za jamii, desturi. 2. Jambo maarufu lililozoeleka kufanywa na jamii fulani. 3. Nywele za shingoni mwa farasi. 4. Upanga wa jogoo. 5. Sehemu ya ardhi iliyoinuka. 6. Kilele cha mlima. 7. Wimbi la bahari. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu urfun عرف lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno arufu lilichukua kutoka Kiarabu maana mahsusi ya nywele ndefu zinazoota kuzunguka shingo ya farasi na kuifanya maana ya nywele ndefu zinazoota kuzunguka shingo ya mnyama kama vile simba na farasi. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |