ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIHAMI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIHAMI' (/showthread.php?tid=2554) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIHAMI' - MwlMaeda - 05-10-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIHAMI' Neno *arihami* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: a-/-wa*] yenye maana ya *ndugu wa upande wa mwanamke.* Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *arihami* limechukuliwa na kutoholewa kutoka neno la Kiarabu *arhaam* ( *soma: arhaamun/arhaaman/arhaamin ارحام )* lililo wingi wa neno la Kiarabu *Rahim (soma: rahimun/rahiman/rahimin رحم)* lenye maana ya *mji wa uzazi.* Katika lugha ya Kiarabu, neno *arhaamun ارحام* huwa linaanza na *dhuu ذو* na kuwa *dhul arhaami ذو الأرحام* lenye maana ya *wenye ujamaa/udugu; ndugu wa karibu* . Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *arhaamun ارحام* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *arihami* liliacha maana ya jumla ya wenye ujamaa/udugu; ndugu wa karibu katika lugha asili - Kiarabu na kuchukua maana mpya ya ndugu wa upande wa mwanamke. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |