ETIMOLOJIA YA NENO 'ZUMARI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ZUMARI' (/showthread.php?tid=2548) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ZUMARI' - MwlMaeda - 05-08-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ZUMARI' Neno *zumari* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya moja ya ala za muziki ambayo utumiwaji wake ni wa kupuliza ili itoe sauti na ambayo ina uwazi mwembamba kwenye sehemu ya kupulizia na mpana mwishoni inakotokea sauti na matundu yanayobadili sauti moja kwenda nyingine; ala ya muziki inayopigwa kwa kupulizwa yenye tundu na umbo jembamba upande wa mdomoni. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *zumari* kwa fasili iliyotolewa katika lugha ya Kiswahili linatokana na neno la Kiarabu *mizmaar*( *soma: mizmaarun/mizmaaran/mizmaarin مزمار )* lenye maana ya ala ya muziki miongoni mwa ala za muziki zenye kupulizwa; ni ala yenye tundu na umbo jembamba iliyo wazi pande mbili na huwa na matundu sita na tundu moja upande unaomuelekea mpulizaji. Neno ' *zumar' (soma: zumarun/zumaran/zumarin زمر)* ni neno la Kiarabu lililo wingi wa neno *zumratun زمرة* lenye maana zifuatazo: 1. Kundi la watu aghalabu marafiki. 2. Mkusanyiko wa bakteria. 3. Aina ya kundi la damu. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *zumari* katika Kiswahili ni natija ya kutamkwa vibaya neno *mizmaar مزمار* au kulipa neno *zumar زمر* maana ya neno *mizmaar مزمار.* *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |