ETIMOLOJIA YA NENO 'ITIFAKI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ITIFAKI' (/showthread.php?tid=2540) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ITIFAKI' - MwlMaeda - 05-04-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ITIFAKI' Neno *itifaki* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo: 1. Maafikiano baina ya pande mbili kuhusu jambo fulani; *maelewano, maridhiano.* 2. Taratibu za kiserikali kushughulikia na kuhudumia shughuli rasmi za viongozi na utawala; *protokali* . *Mfano* : Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imezungumzia uanzishwaji wa Kamisheni ya Kiswahili. Katika lugha ya Kiarabu neno *itifaki* linatokana na neno la Kiarabu *ittifaaq (soma: ittifaaqun/ittifaaqan/ittifaaqin اتفاق)* lenye maana zifuatazo: 1. Maelewano au mapatano baina ya nchi mbili ya kumaliza mzozo. 2. Maafikiano baina ya pande mbili kuhusu jambo fulani; *mkataba*. 3. Hali ambapo mambo au matukio mawili au zaidi hutokea kwa wakati mmoja bila ya kupangwa au kutarajiwa; *sadfa*. Kinachodhihiri ni kuwa neno *ittifaaq اتفاق* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *itifaki* maana ya *mapatano; mkataba* haikubadilika bali Waswahili waliongeza maana ya *protokali* ambapo Waarabu hutumia neno ' *maraasimu* ' ( *soma: maraasimu/maraasima مراسم)*. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |