ETIMOLOJIA YA NENO 'ANUANI/ANWANI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ANUANI/ANWANI' (/showthread.php?tid=2526) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ANUANI/ANWANI' - MwlMaeda - 04-23-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ANUANI/ANWANI' Neno *anuani/anwani* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo: 1. Maelezo ya mahali ambapo mtu huishi au hufanya kazi, ambayo husaidia kumfikishia kufurushi au barua iliyotumwa hasa kwa njia ya posta; mahali panapotumiwa kufikishia barua. 2. Akaunti ya mtandao wa kutuma na kupokea barua kupitia mfumo wa intaneti. 3. Mada au jina la kitabu. Katika lugha ya Kiarabu neno *anuani/anwani* linatokana na neno la Kiarabu *unwaaanu (soma: unwaanun/unwaanan/unwaanin عنوان)* lenye maana zifuatazo: 1. Kinachotoa utambulisho wa kipekee kwa kitu usiofanana na mwengine. Kwa mfano: *Unwaanul Kitaabi عنوان الكتاب* anuani ya kitabu. 2. Maandishi yaliyodhihirishwa yanayoelezea kilichofichwa. 3. Maandishi yanayoandikwa juu ya bahasha kubainisha anayepelekewa na makazi yake. Kinachodhihiri ni kuwa neno *unwaanun عنوان* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *anuani/anwani* maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu inayohusu utambulisho haikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |