MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAIRI'' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAIRI'' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAIRI'' (/showthread.php?tid=2501)

ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAIRI'' - MwlMaeda - 04-05-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAIRI''

Neno *shairi*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: li-/ya-, wingi: mashairi]* yenye maana ya mtungo wenye muundo na lugha ya kisanii na unaofuata utaratibu wa vina na mizani, hisi au tukio juu ya maisha au jambo na hufuata utaratibu maalumu wa urari na muwala unaozingatia kanuni za utunzi wa mashairi yanayohusika, tungo yenye lugha ya kisanii, vina na mizani, urari na muwala maalumu katika uelezeaji wa jambo kwa kuzingatia kanuni za ubunifu wa mashairi yanayohusika.

Neno *shairi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *shi'iri* ( *soma: shi'irun/shi'iran/shi'irin شعر)*  ambalo ni nomino iliyo katika umoja (wingi wake ni neno *ash'aar  اشعار*).
Neno hili *shi'irun شعر* lina maana zifuatazo:

1. Maneno yenye urari uliokusudiwa.

2. Katika istilahi za watu wa Mantiki ni msemo unaojumuisha mambo ya kufikirika, unaokusudiwa kuraghibisha au kuhofisha, kama vile msemo: *divai ni yakuti* safi na *asali ni matapishi ya nyuki.*

3. *Shairi-Nathari*, *Ash-Shi'irul Manthuur الشعر المنثور*, usemi fasaha unaozingatia mzamo wa mawazo na mvuto *bila ya kuzingatia mizani.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *shi'irun شعر* lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *shairi* lilichukua maana ya *tungo yenye kuzingatia kanuni za Arudhi.*

*TANBIHI:*
Neno *shi'irun  شعر* katika Kiarabu limelibeba shairi linalozingatia kanuni za Arudhi na lile lisilozingatia kanuni hizo ambalo wamelipa jina la *chotara wa nudhumu na nathari* *shairi-nathari, ash-shi'irul manthuur الشعر المنثور*.

Wanataaluma wa lugha ya Kiarabu wanasisitiza kuwa Ushairi ni ule unaozingatia kanuni za utunzi wa mashairi (Arudhi) kama zilivyoasisiwa na Mwanazuoni Malenga wa Kiiraq (Basra) Alkhalili bin Ahmad Al-Farahidi aliyezaliwa nchini Oman mwaka 718 AD na kutawafu mwaka 791 AD.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*