MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALHAJ', 'HAJI' NA 'HAJATI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALHAJ', 'HAJI' NA 'HAJATI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALHAJ', 'HAJI' NA 'HAJATI' (/showthread.php?tid=2496)

ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALHAJ', 'HAJI' NA 'HAJATI' - MwlMaeda - 04-03-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALHAJ', 'HAJI' NA 'HAJATI'

Neno *alhaji* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: a-/wa-, wingi: ma-alhaj]*  yenye maana zifuatazo:

1.  Jina la heshima linalotangulia jina halisi la Muislamu aliyekwisha kwenda Makka kuhiji.

2. Mwanamume aliyehiji Makka; *haji.*

Neno *hajati* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: a-/wa-, wingi: mahajati]*  yenye maana ya mwanamke aliyehiji Makka.

Katika lugha ya Kiarabu, neno *alhaji/haji* *(soma: alhaajju/alhaajja/alhaajji, haajjun/haajjan/haajjin)* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Mtu aliyetembelea Al-Kaaba iliyopo Makka kwa nia ya kutekeleza ibada ya Hija. Wingi wa neno hili katika Kiarabu ni *hujjaajun na hajiijun حجاج/حجيج* .

2. Mti wenye miba unaohimili kukosa maji na mizizi yake huenda mbali ardhini. Huitwa *shaukatul Jamaal mwiba wa ngamia (camel thorn)*. Nchini Iraq hujulikana kwa jina la *Al-aaquul العاقول*.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *alhaaj/haajun الحاج/حاج* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *alhaji/haji* maana yake katika lugha yake asili Kiarabu haikubadilika na maana ya mti wenye miba haikuzingatiwa.

Kamusi ya Karne ya 21 imesajili neno *hujaji* ( wingi wa neno *haji* katika Kiarabu) kuwa kisawe cha neno *haji* na wingi wake kuwa *mahujaji*.

Ingawa maelezo 'neno alhaji ni  jina la heshima linalotangulia jina halisi la Muislamu aliyekwisha kwenda Makka kuhiji' yanaonesha kumuhusu Muislamu yeyote yule mwanamume na mwanamke, Waswahili hawalitumii kwa mwanamke bali humuita *hajati*.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*