ETIMOLOJIA YA NENO 'AFUENI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFUENI' (/showthread.php?tid=2467) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFUENI' - MwlMaeda - 03-26-2022 *HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFUENI'.* Neno *afueni* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/i-]* yenye maana zifuatazo: 1. Hali nzuri ya afya inayomrejea mtu baada ya kuugua au kuwa katika maumivu. 2. Unafuu aupatao mtu baada ya kuondokewa au kupungukiwa na ugumu au uzito wa jambo; nafuu. 3. Tendo la kupungua kwa maradhi, hali ya kupata hujambo. *Nahau*: *pata afueni:* pata nafuu. Kamusi Kuu ya Kiswahili imetoa fasili ya neno hili kwa kuandika: *tazama ahueni.* Katika lugha ya Kiarabu, neno *afueni* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *afwan*( *soma: afwun/afwan/afwin عفو)*, nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Wema, ubora. 2. Ziada ya mali isiyomsumbua mwenye mali kuitoa. 3. Msamaha kama ule anaoutoa raisi wa nchi kwa wafungwa. 4. Tamko la kuomba msamaha; *afwan! عفوا* samahani. 5. Kufanya jambo, kama vile kutoa hotuba, bila ya kujiandaa. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *afwan عفوا* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *afueni* limefanywa *kisawe* cha neno *ahueni* na kuacha maana zake katika lugha asili - Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |