ETIMOLOJIA YA MANENO 'MAAFA' NA 'ALAKATI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'MAAFA' NA 'ALAKATI' (/showthread.php?tid=2463) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'MAAFA' NA 'ALAKATI' - MwlMaeda - 03-18-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'MAAFA' NA 'ALAKATI' Neno maafa katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: ya-/ya-] yenye maana zifuatazo: 1. Madhara makubwa mfano uharibifu wa mali na vifo, yanayosababishwa na majanga kama mafuriko, moto, ukame au magonjwa. 2. Tukio la kudhuru au kutia hasara. Neno alakati katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] iliyo kisawe cha neno maafa. Katika lugha ya Kiarabu, neno maafa limetoholewa kutoka neno la Kiarabu ' aafa' (soma: aafatun/aafatan/ aafatin آفة) lenye maana ya chenye kuharibu mfano shamba la mazao kama vile wadudu au magonjwa ya mimea na mengineyo. Na neno alakati limetokana na neno la Kiarabu halakaat (soma: halakaatun/halalaatin هلكات) wingi wa neno la Kiarabu halaka (soma: halakatun/halakatan/halakatin هلكة ) lenye maana ya _kuangamia . Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu aafatun آفة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno maafa maana yake katika lugha yake asili Kiarabu haikubadilika ingawa Waswahili walilifanye neno alakati lililotoholewa kutoka neno la Kiarabu halakaatun هلكة kuwa kisawe cha neno la Kiswahili maafa . Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |