ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO' (/showthread.php?tid=2455) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO' - MwlMaeda - 03-13-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO' Neno *aridhio* katika lugha Kiswahili ni *Nomino* inayotokana na kitenzi elekezi *aridh.i* chenye maana zifuatazo: 1. Ingilia mtu katika jambo analolisimamia. *Mnyumbuliko: aridhia, aridhika aridhiwa, aridhiana, aridhisha.* *Visawe: kera, sumbua, udhi, ghasi.* 2. Orodhesha vitu; weka vitu kwa mpangilio kuanzia kimoja hadi kingine. 3. Soma kwa kukariri bila ya kuangalia maandishi mbele ya mwalimu aghalabu Qur'aan Tukufu. 4. Kitenzi elekezi *aridhi.a* fafanua jambo fulani. *Visawe: arifu, juvya, fahamisha, julisha.* Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *aridhi* linafanana na kitenzi cha Kiarabu *aaridh عارض* kitenzi cha kuamrisha/kutaka tendo kutendeka, kinachotokana na kitenzi cha msingi cha Kiarabu *aaradhwa عارض* chenye maana zifuatazo: 1. Ingilia mtu kati kwa kuhoji au kupinga anachokisema. 2. Epuka jambo fulani. 3. Yapinge maandishi kwa kutoa maandishi dhidi yake. 4. Tembea pembezoni mwa njia. 5. Dhihirisha/weka wazi jambo/taarifa fulani; soma kwa kukariri bila ya kuangalia maandishi. 6. Onesha kitu fulani kwa wengine. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiswahili *aridhio* halina mfano wake katika Kiarabu na *si neno la Kiarabu* bali limebuniwa kutokana na kitenzi cha Kiarabu *aaridhi عارض* kinachotokana na kitenzi cha msingi cha Kiarabu *aaradha عارض* kilichofafanuliwa hapo juu. Katika Kiarabu tendo-jina *masdar مصدر* la kitenzi cha Kiarabu *aaradha* ni *muaradha معارضة* lenye maana ya kuweka wazi taarifa; *onesho* . *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |