ETIMOLOJIA YA NENO 'DIWANI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'DIWANI' (/showthread.php?tid=2444) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'DIWANI' - MwlMaeda - 03-05-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'DIWANI' Neno diwani katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. Nomino [Ngeli: a-/wa- wingi: madiwani] mjumbe aliyechaguliwa na wananchi wa kata ili awawakilishe katika baraza la jiji, manispaa au halmashauri ya wilaya. 2. Nomino [Ngeli: i-/zi-] kitabu cha mashairi chenye mkusanyiko wa mashairi ya mshairi mmoja Katika lugha ya Kiarabu, neno hili diwani( soma: diiwaanun/diiwaaanan/fiiwaanin ديوان) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Daftari linalohifadhi majina ya askari wapiganaji, wanapopatika na shughuli wanazozifanya na majina ya wafadhili. 2. Kitabu chenye mkusanyiko wa mashairi. 3. Kitabu chochote kile. 4. Ofisi/Afisi. 5. Ofisi/Afisi inayoshughulikia mambo ya utawala; mahakama. 6. Katika nchi za Kiarabu, ofisi ndogo ya wizara inayoshughulikia mambo maalumu. 7. Lugha rasmi ya kiserikali itumikayo katika ofisi/afisi za serikali. Kinachodhihiri ni kuwa neno ya Kiarabu diiwaanun/diiwaaanan/fiiwaanin ديوان) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno diwani lilichukua kutoka lugha yake ya asili - Kiarabu maana ya Kitabu chenye mkusanyiko wa mashairi na kupewa maana mpya ya mjumbe aliyechaguliwa na wananchi wa kata ili awawakilishe katika baraza la jiji, manispaa au halmashauri ya wilaya. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |