ETIMOLOJIA YA NENO 'AJABU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AJABU' (/showthread.php?tid=2421) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AJABU' - MwlMaeda - 03-03-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJABU' Neno *ajabu* katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Nomino [Ngeli: i-/ya- wingi: maajavu]* kitu, kiumbe au jambo linaloshangaza. 2. *Nomino [Ngeli: i-/ya- wingi: maajabu]* kitu au jambo lisilomithilika wala kuaminika. 3. *Kivumushi* . (i) -a pekee, -iso kawaida, -a kioja, -a kigeni (ii) -isomithilika wala kuaminika, -a kimiujiza. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ajabu*( *soma: ajabun/ajaban/ahabin عجب)* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Mshangao, kukishangaa kitu kutokana na kutokuwa na mazoea nacho. 2. Mapenzi, hali ya kukipenda kitu kisichostahili kupendwa, moyo kuvutwa na kukiona kibaya kuwa kizuri. 3. (Kutoka kwa Mwenyeezi Mungu) ridhaa. Kinachodhihiri ni kuwa neno ya Kiarabu *ajabun/ajaban/ajabin عجب)* likipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ajabu* lilichukua kutoka lugha ya asili - Kiarabu maana inayohusu mshangao, upekee na kupendeza na kuacha maana ya kiibada inayohusu ridhaa ya Mwenyeezi Mungu kwa waja wake. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |