ETIMOLOJIA YA MANENO 'KISHAUFU' NA 'KIPINI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'KISHAUFU' NA 'KIPINI' (/showthread.php?tid=2415) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'KISHAUFU' NA 'KIPINI' - MwlMaeda - 02-28-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'KISHAUFU' NA 'KIPINI' Neno *kishaufu* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: ki-/vi- wingi: vishaufu]* ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Pambo linalovaliwa na wanawake kwa kulining'iniza puani; *hazima* . 2. Kikuku anachofungwa mnyama puani; *shemere* . Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *kishaufu* ( *soma: shawfun/shawfan/shawfin شوف)* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Chombo kinachotumika kusawazisha ardhi iliyolimwa. 2. Jina *(masdar)* linalotokana na kitenzi cha Kiarabu *shaafa/shawwafa شاف/ شوف* lenye maana ya kuona, kutazama na kupamba. Waarabu husema: *Shawwafahul Jaariya, شوفه الجارية: زينها* Amempamba. 3. Pambo linalompendezesha mwanamke. Neno *kipini* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: ki-/vi- wingi: vipini]* ni nomino yenye maana ya pambo linalovaliwa puani; pambo linalotengenezwa kwa chuma, madini, pembe, mti au plastiki linalovaliwa na wanawake puani. Etimolojia ya neno kipini ni lugha ya Kiingereza na huko hutambuliwa kwa jina la *nose pin/nose ring.* Desturi ya kuvaa vipini inarejea nchini Australia miaka 44,000 Kabla ya Kristo ambapo watu wa jamii ya wazawa wa asili wa Australia, Waaborigini (Aboriginal) walikuwa wakitengeneza vipini na kuvivaa. Desturi hii iliyoingia Ulimwengu wa Kimagharibi kunako Karne ya 20 imekuwepo kwa maelfu ya miaka katika maeneo kama vile Mashariki ya Kati, India na Afrika. Kwa kweli, kutoboa pua ni aina ya pili ya kutoboa mwili iliyo maarufu baada ya kutoboa masikio. Ifahamike kuwa kipini/kikuku huvalishwa wanyama puani na Waswahili hukiita *shemere* *Nahau:* *Tia mtu shemere:* tawala mtu hata kumfanya afanye kila analoambiwa pasi na kuuliza swali. Kinachodhihiri ni kuwa wakati neno la Kiarabu *shawfun/shawfan/shawfin شوف)* ambalo moja ya maana zake ni pambo linalompendezesha mwanamke lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa *kishaufu* lilichukua maana ya pambo linalovaliwa na wanawake kwa kulining'iniza puani. Huitwa pia hazama. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |