ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA' (/showthread.php?tid=2410) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA' - MwlMaeda - 02-27-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA' Neno *arafa* katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Nomino [Ngeli: i-/i-]* siku ya tisa ya mwezi Dhulhija (Mfungo Tatu) katika Kalenda ya Kiislamu - Hijiriyyah. 2. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* ujumbe mfupi wa maandishi unaotumwa na kupokewa katika simu ya mkononi. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *arafa*( *soma: arafatu/arafata عرفة)* ni nomino ya Kiarabu, wingi wake ni *arafaat عرفات* yenye maana zifuatazo: 1. Mahali penye mchanga paliponyanyuka. 2. Kizuizi kati ya vitu viwili. 3. Tendo-jina la Kitenzi cha Kiarabu *arafa/ya-arifu عرف/يعرف* chenye maana ya : -metafuta habari, -meuliza. 4. Siku ya tisa ya mwezi Dhul-Hijjah (Mfungo Tatu) katika Kalenda ya Kiislamu - Hijiriyyah. 5. Jina la mlima maarufu karibu na mji wa Makkah, nchini Saudi Arabia. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *arafatu/arafata/عرفة)* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *arafa* lilichukua kutoka lugha ya asili - Kiarabu maana ya *siku ya tisa ya mwezi Dhul-Hijjah (Mfungo Tatu)* na kubeba maana mpya: *ujumbe mfupi wa maandishi inaotumwa na kupokewa katika simu ya mkononi.* *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |