MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI' - Printable Version
|

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI' (/showthread.php?tid=2409)
|
ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI' - MwlMaeda - 02-26-2022
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI'
Neno *akisami* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:
1. Sehemu ya kitu, umbo au tarakimu kama vile robo (1/4), theluthi (1/3), au nusu (1/2).
2. Umbo au namba isiyo kamili.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *aksami*( *soma: aqsaamun/aqsaaman/aqsaamin اقسام)* ni nomino ya Kiarabu, wingi wa neno la Kiarabu *qismun قسم* lenye maana ya fungu au sehemu ya kitu kilichogawanywa.
Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *aqsaamun/aqsaaman/aqsaamin أقسام)* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *aksami* maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*
|