ETIMOLOJIA YA NENO 'MEMOSAS' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'MEMOSAS' (/showthread.php?tid=2399) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'MEMOSAS' - MwlMaeda - 02-14-2022 KWA KUTEKELEZA AMRI YA WAZEE WANGU WALIOTAKA ETIMOLOJIA YA NENO 'MEMOSAS'. *HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MIMOSAS'.* Neno *mimosas* katika lugha ya Kiingereza ni wingi wa neno *mimosa* *(nomino)* yenye maana zifuatazo: 1. Jenasi yoyote (Mimosa) ya miti, vichaka na mimea ya jamii ya mikunde inayotokea katika maeneo ya tropiki na joto na kwa kawaida huwa na majani yenye michomo na vichwa vya maua madogo meupe au waridi. 2. Mti wa hariri. 3: kinywaji mchanganyiko kinachojumuisha champagne na juisi ya machungwa. Kuna Sikukuu ya Kitaifa isiyo rasmi ambayo husheherekewa nchini Kroshia (Crotia) tarehe 16 Mei kila mwaka kwa ajili ya kukitukuza kinywaji hiki maarufu na kinachopendwa sana na wazee. Wataalamu wa Etimolojia wanadai kuwa asili ya neno hili ni Hispania (Kihispanyola) na kwamba lilianza kuwa mashuhuri nchini Uingereza baada ya kuingia kinywaji hiki mwaka 1921. Kinachodhiri ni kuwa maana ya msitu na miti yenye maua ya njano kadhalika kinywaji cha rangi ya njano, kwa ujumla wake, ni mazingira rafiki na sadifu kwa yale yaliyojiri na yatakayoendelea kujiri miongoni mwa matukio duniani. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |